The House of Favourite Newspapers

Pialali Amchakaza Mhindi Bagamoyo (Video)

 

BONDIA wa ngumi za kulipwa  nchini, Idd Pialali amefanikiwa kushinda ubingwa wa kimataifa baada ya kuchakaza mpinzani wake, Shiva Gurgaon raia wa India kwa pointi katika pambano la raundi kumi lililofanyikauta  jana usiku  kwenye Ukumbi wa Travel Lodge, Bagamoyo mkoani  Pwani.

 

Katika pambano hilo Pialali ambaye anashikiria mkanda wa ubingwa Global TV  Afrika Mashariki na Kati, ameshinda kwa ushindi wa majaji wote watatu dhidi ya mpinzani wake ambapo jaji wa kwanza Laszlo Fejes alitoa pointi kwa  98-90,  Agapeter Mnazareth 98-91 na  Robert Kasiga 97-93.

Kufuatia ushindi huo Pialali amewashukuru Watanzania na mashabiki wake kujitokeza na kuweza kumsapoti katika pambano hilo huku akitoa ahadi ya kuhakikisha anaileta mikanda mikubwa duniani ya mchezo huo.

 

“Nawashukuru Watanzania kwa sapoti kubwa ambayo wameweza kunipa katika pambano hili kwa sababu mpinzani wangu hakuwa mtu wa kubeza kutokana na uiamara mkubwa ambao alikuwa nao katika raundi zote.

 

“Nilipanga nimalize pambano mapema lakini haikuwezekana kwa kuwa mpinzani wangu alikuwa mjanja kuingia kwenye mitego yangu lakini kikubwa nashukuru kwa ushindi  huu pia ni nimshukuru waziri Mwakyembe kwa kuweza kuangalia mchezo kwa jicho lengine na mimi nitahakikisha mikanda mikubwa inakuja nchini,” alisema Pialali.

Comments are closed.