The House of Favourite Newspapers

Zanzibar: Mtalii Afa Chini ya Bahari Akimchumbia Mpenzi Wake

MTALII mmoja aliyejulikana kwa jina la Steven Weber Jr, amefariki dunia hivi karibuni akiwa chini ya bahari alikoenda kumvisha pete mchumba wake, Kenesha Antoine, wakati wa likizo.

 

Mtandao wa Sky News, umesema Weber na Kenesha walikuwa wakiishi katika hoteli moja ya mbao ambayo ipo chini ya maji baharini huko Zanzibar ili kuwawezesha kuona kilichopo majini.

 

Picha zimeonyesha wakati Weber, mkazi wa Baton Rounge, Luoisiana, Marekani, aliogelea hadi katika dirisha moja lililopo chini ya maji kabla ya kushika karatasi akimuomba Antoine akubali kufunga naye ndoa.

 

Karatasi hiyo ilisoma kwa tafsiri isiyo rasmi: “Siwezi kuzuia pumzi zangu kwa muda mrefu ili kukwambia kila kitu ninachokupendea lakini kila kitu ninachokupendea nakupenda kila siku”.

Weber baadaye aliibadilisha karatasi hiyo ili kuonyesha maneno aliyokuwa ameandika upande mwingine yaliyosema: “Je tafadhali unaweza kuwa mke wangu? Utafunga ndoa nami???”

 

Baadaye, kwa mujibu wa mtandao huo,  alitoa pete ya uchumba mfukoni mwake kabla ya kuogelea na kuondoka eneo hilo. Bi Antoine naye alichapisha picha za tukio hilo katika mtandao wa Facebook ambapo anaonekana akifurahia kwa  tamko lake la: “Ndiyo! Ndiyo! Ndiyo!”

 

Lakini mrembo huyo baadaye alichapisha habari mbaya kwamba mpenzi wake amefariki. Alisema hakurudi akiwa mzima baada ya kuogelea baharini. Wizara ya masuala ya kigeni nchini Marekani ilisema kwamba mtalii mmoja wa Marekani amefariki nchini Tanzania lakini hakuna maelezo zaidi yaliyoripotiwa.

Comments are closed.