The House of Favourite Newspapers

MWALIMU LONGIDO AZINDUA KITABU CHA TANZANIA YA SASA

Afisa Tawala wilaya ya Longido, Malack Tateni (kushoto) akiwa na mtunzi wa kitabu cha Tanzania ya sasa mwalimu Grace Sarakikya
Wadau mbalimbali wakikabidhiwa kitabu hicho na Afisa Tawala Wilaya ya Longido, Malack Tateni(kulia) baada ya uzinduzi.
Tateni akiendelea kuwakabidhi vitabu.
…Tateni (kulia) akiendelea kuwakabidhi vitabu wadau wa elimu kitabu kilichoandikwa na Grace.

 

JAMII ya wafugaji wilayani Longido mkoani Arusha imehamasishwa kujitoa  kwa wingi na kuwekeza katika elimu ya watoto wao, na kuachana na mila na desturi zilizopitwa na wakati za kuwaozesha watoto wa kike katika umri mdogo.

 

 

Hayo yalisemwa na Afisa Tawala wilaya ya Longido, Malack Tateni wakati akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kitabu cha “Tanzania ya sasa ” uliofanyika wilayani Longido kilichoandikwa na Mwalimu Grace Sarakikya.

 

 

Tateni alisema kuwa, wilaya ya Longido ni wilaya ya kifugaji  ambapo suala zima la mwamko wa elimu ndo linaanza kuonekana sasa hivi kutokana na jitihada mbalimbali zinazofanywa za kuhamasisha jamii hiyo kuwekeza katika elimu ya watoto wao bila kubagua mtoto wa kike au wa kiume.

 

 

Aidha alizitaka jamii hiyo kubadilika sasa na kuchangamkia fursa ya elimu bure inayotolewa na serikali  ya awamu  ya tano  kwa kupeleka watoto wao shuleni  kwa wingi na hatimaye kuweza kupata wasomi wengi zaidi huku akiwataka kuacha mila na desturi zilizokuwepo.

 

 

“Nampongeza sana mwalimu huyu kwa kuamua kuja na kitabu hiki  ambacho kinaelezea kazi alizofanya Rais kwa kipindi cha  miaka mitatu ili kila mmoja aweze kujua hususani kwa wananchi waliopo vijijini ambapo radio wala television haziwafikiii na kupitia kitabu hiki wataweza kujionea mambo makubwa  aliyoyafanya Rais Magufuli.”alisema Tateni.

 

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho, Mwalimu Grace Sarakikya alisema kuwa,lengo la kuandika kitabu hicho  chenye jina la “Tanzania ya sasa” ni kutokana na kuwepo kwa majadiliano yaliyo hasi  kuhusu serikali ya awamu ya tano kwa miongoni  mwa watu ndipo alipoamua kukiandika kitabu hicho kinachoonyesha mambo aliyoyafanya Rais Magufuli kwa kipindi kichache akiwa madarakani.

 

 

Alisema kuwa,kitabu hiki kitaweza kuondoa fikra na mawazo batili ya baadhi ya watanzania wanaofikiri kuwa Tanzania haijabadilika na kuona serikali haifanyi kitu,ambapo kupitia kitabu hicho watatambua juhudi zilizofanyika na mambo mengi yaliyotekelezwa ndani ya miaka  mitatu ya serikali hii ya uongozi makini.

 

 

Alitaja changamoto inayomkabili kuwa ni pamoja na rasilimali fedha kwani lengo la kuandika kitabu hicho ni kuwafikia watanzania waliopo kila kona ya nchi ili waweze kutambua mambo ambayo Mh.Rais ameyafanya katika Tanzania hii, huku akiomba mchango wa Tshs 1 Milioni ili aweze  kutoa nakala za vitabu vya kutosha kwa ajili ya kuvisambaza kwa watanzania.

 

 

Kwa upande  wa Afisa biashara  wilaya ya Longido ,Paulo Parmeti alisema kuwa,kitendo kilichofanywa na mwalimu Grace kitatoa fursa kwa wanajamii wa Longido kutambua umuhimu  wa elimu kwani bado wengi wao hawatambui  umuhimu  wake hasa katika swala zima la kuwasomesha watoto wa kike.

 

 

Naye mwananchi mwingine, Exaud Sarakikya aliitaka jamii yenye  uwezo wa kuzitangaza kazi zinazofanywa na viongozi wetu  kuendelea kufanya hivyo kwa maandishi ili ziweze kuwafikia watu wengi zaidi.

Comments are closed.