The House of Favourite Newspapers

Zanzibar Stars, Bella kukiwasha Dar Live

0
King Of The Best Melodies, Christian Bella ‘Obama’ .

KWA mara ya kwanza katika sekta ya burudani nchini, King Of The Best Melodies, Christian Bella ‘Obama’ pamoja na kundi kongwe la Muziki wa Taarab nchini, Zanzibar Stars wanatarajiwa kukiwasha Septemba 3, mwaka huu ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.

 

Akizungumza na Risasi Vibes, Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo alisema kuwa usiku huo Zanzibar Stars litakuwa chini ya wakali kibao akiwemo Bi.Mwanahawa na Jokha Kassim.

“Utakuwa usiku wa weka kitu toa kitu mwanzo mwisho. Mashabiki na wapenda Muziki wa Mwambao wote hii si ya kukosa kwani Zanzibar Stars itashusha mtaalamu wa sauti za kumtoa nyoka pangoni, Mosi Suleiman huku safu ya kinanda Ally Jay akifanya yote na mbele kabisa atakuwepo Issa Kamongo utakosaje sasa?” alisema Mbizo na kuongeza;

“Mbali na uwepo wa Zanzibar Stars, kutakuwa tena na Bella mzee wa masauti ambaye atapagawisha kwa ngoma zake zote kali kuanzia Nani Kama Mama, Safari Siyo Kifo, Nashindwa na nyingine nyingi huku naye mkali wa Bongo Fleva, Pam D akikinukisha kwa ngoma zake za Popolipopo, Nimempata na Ngoma Droo akiwa na Bella.”

 

Stori: Risasi Vibes

 

BREAKING NEWS: Kauli ya Kwanza ya ROMA Baada ya Kutua Bongo Akitokea Zimbabwe

Leave A Reply