The House of Favourite Newspapers

 ZARI AMKINGIA KIFUA MPENZI WA VANESSA

BAADA ya mwanamuziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee ‘V-Money’ kuthibitisha kuwa kwenye penzi jipya na staa wa Hollywood, Marekani mwenye asili ya Nigeria, Rotimi, jamaa huyo amekuwa akipondwa kinoma mitandaoni, kiasi cha kumfanya mwanamama Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kumkingia kifua.

Wakati penzi hilo likiwa ndiyo habari ya mjini, baadhi ya watu wa mitandaoni hasa Instagram waliponda ‘kapo’ hiyo huku wakidai Rotimi ana pua kubwa, jambo lililomfanya Zari ambaye ni ‘eksi’ wa Diamond kujitosa kumtetea.

Katika moja ya posti za kumponda jamaa huyo kwenye Instagram, Zari aliandika; “Ndiyo maana wanaume tunawaficha siku hizi kwa sababu mashemeji wa Instagram hawajatulia kabisa, hakuna mtu sahihi hivyo mwacheni Vee (Vanessa).”

STORI: NEEMA ADRIAN, DAR

Comments are closed.