The House of Favourite Newspapers

Zari Atua Bongo, Atoa kauli ya Kumkacha Mpenzi Wake – Video

0
Zari akiwasili Airport.

MFANYABIASHARA Zari The Bosslady ametua Tanzania, leo jioni  Septemba 13, akitokea nchini Afrika Kusini kwaajili ya kuzindua duka jipya la bidhaa za nguo, Danube lililopo Mlimani City jijini hapa.

Zari ametua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akiwa bila mtoto wake mdogo Nillan kitendo ambacho kimeonyesha huwenda mrembo huyo hajafika kwa ajili ya mpenzi wake na ni kwa muda mchache.

…Akiondoka Airport.

Akiongea na waandishi wa habari baada ya kuwasili, Zari amesema amekuja nchini kwa ajili ya uzinduzi wa duka la Danube na si kitu kingine

“Nimekuja Tanzania kama balozi wa Danube. Kwahiyo nashukuru kwa upendo wetu, na tuendelee kutumia bidhaa za Danube,” alisema Zari.

Zari amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi Mlimani City siku ya kesho kwa ajili ya uzinduzi wa duka hilo. Wawili hao waliingia kwenye mgogoro mzito wa mapenzi baada ya mpenzi wake kuchepuka na mwanamitindo, Hamisa Mobetto na kuzaa naye mtoto mmoja.

Zari Atua Bongo, Amkacha Baby Wake

Leave A Reply