The House of Favourite Newspapers

Zari Awaonya Mashabiki Zake na Matapeli

0
Zarina Hassan ‘Zari’.

Mzazi mwenza wa Msanii wa Bongofleva nchini, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarina Hassan ‘Zari’ amewaonya mashabiki zake kuwa makini na baadhi ya matapeli wa mitandao wanaotumia jina lake kutapeli fedha.

 

Kupitia akaunti yake ya mtandao wa Instagram, Mama huyo wa watoto watano ambaye pia ni mfanyabiashara anayeishi Afrika Kusini aliwaonya mashabiki kwamba hausiki kwa chochote na wala hatowajibika kwa watu wasio waaminifu wanaojifanya kuwa yeye.

Kwa mujibu wa Zari, jamaa aliyejifanya kuwa yeye (Zari) alidaiwa kukopa pesa kutoka kwa mmoja wa mashabiki wake na akashindwa kuirejesha.

 

Mmoja wa mashabiki hao alipakia mtandaoni barua ya madai ambayo alidai amemlipa Zari Sh milioni mbili.

“Nitaendelea kukuonya, ibiwa kwa sababu ya akili zako ndogo. Hauwezi kutuma pesa kwa watu usiowajua… Wewe ni mjinga,” aliandika Zari.

Msosholist huyo alisema atawafichua wale wanaochafua jina lake zuri huku akisema kwamba hajawahi kuomba msaada wa kifedha.

Stori na Mushi Gabriel

Leave A Reply