The House of Favourite Newspapers

Zari, Mobeto Kukutana uso kwa uso Uganda

Hamisa Hassan Mobeto.

Kama ulifikiri kuwa Baby mama wa mbongo fleva maarufu,  Zarinah Hassa ‘The Boss Lady’ na Hamisa Hassan  Mobeto bifu lao limetulia au kuisha kabisa utakuwa umekosea.

Zari na Hamisa wamekuwa wakiripotiwa kutoelewana na kurushiana vijembe katika mtandao tangu Hamisa alipozaa na msanii huyo asiyekuwa na nidhamu na zipu yake wakati akijua fika Zari bado ameweka kambi kimapenzi.

Sasa Hamisa na Zari si kwamba wanaviambiana tu kwenye mitandao, bifu lao limeenda mbali zaidi lakini katika njia ambayo ni nzuri.

Zarinah Hassa ‘The Boss Lady’.

Wakati Zari akitarajia kufanya event yake ya Zari All White Party nchini Uganda nyumbani kwao December 21 mwaka huu, siku hiyohiyo Hamisa naye amealikwa kwenye Tamasha la Girls Power ambalo litafanyika siku moja na party ta Zari, jambo ambalo linavuta hisia za wadau na wapenzi wengi wa burudani.

 

Comments are closed.