The House of Favourite Newspapers

Zari Kujifungua Soon, Apelekwa Hospitali Sauz, Diamond na Mama Yake Waungana Naye

zari-sauz-1  zari-sauz-2 zari-sauz-3 zari-sauz-4

HABARI ya town kwa sasa ni kuhusu kujifungua kwa mpenzi wa mwanamuziki nguli wa Bongo Fleva nchini Diamond Platnumz, Zarinah Hassan a.k.a Mama Tiffah.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diamond anayetarajia kupata mtoto wa kiume ametupia video inayomuonesha Zari akiwasili katika hospitali ambayo haikutajwa jina iliyopo nchini Afrika Kusini ikionyesha dhahiri kwamba yupo tayari kujifungua mtoto wa pili wa nguli huyo wa Bongo Fleva ambapo aliandika ni Jina gani vile mmesema nimpe?

Which Name did you guys said, that i should call my Son…? ADD ME ON SNAPCHAT TO WATCH FUUL PROCESS: Dplatnumz Dplatnumz

A video posted by Chibu Dangote (@diamondplatnumz) on

Zari alikuwa kwenye kiti cha kubebea wagonjwa “Wheel Chair” wakati akifikishwa hospitalini hapo huku pembeni akiwepo mama mkwe wake, Sandra Kassim ambaye ni mama mzazi wa Diamond pamoja na wahudumu wa hospitali hiyo.

zari-sauz-2

Mapema leo, staa huyo aliweka picha yake akiambatana na mama yake mzazi wakiwa kwenye ndege wakielekea Afrika Kusini kwa ajili ya kuwa karibu na Zari huku akiandika maneno yafuatayo;

Na mama Chibu D Chibu De … flying to our new Second home, South africa For my New Born… #MiniMe #ChibuJunior #YoungSimba #YoungLion Ungependa nimpe jina gani eti?😊

halotel-strip-1-1

Comments are closed.