The House of Favourite Newspapers

Zawadi za ligi Kuu ya Vodacom kutolewa mwezi ujao

0

001.PR

Mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, Yanga African Sports Club, Azam FC, Simba Sports Club na Prisons, Pamoja na Mchezaji Bora, Mfungaji Bora wa Ligi na Kocha Bora wa msimu huu ulioisha watakabidhiwa zawadi zao mapema mwezi ujao na Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania ambayo ni  Mdhamini Mkuu wa Ligi hiyo.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu amesema kuwa ucheleweshaji wa kutoa zawadi hizo baada ya kumalizika  msimu wa ligi hiyo mwezi uliopita umetokana na baadhi ya timu zinazoshiriki kwenye mechi za mashindano ya kimataifa kama vile mashindano ya kombe la shirikisho barani Afrika na kuingia kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

“Tunaomba radhi kwa  timu husika, wachezaji na wadau wa soka kwa zoezi hili kuchelewa ila tunawahakikishia kuwa  zawadi ziko tayari na zitakabidhiwa  mapema mwezi ujao”. Alisema Nkurlu.

Pia alishukuru wadau wote waliofanikisha ligi hiyo hadi kufikia mwisho ambapo timu yanga ya jijini Dar es Salaam iliibuka tena bingwa kwa mwaka huu “Licha ya changamoto zinazoendeleza kujitokeza katika ligi  yapo mafanikio makubwa na ligi hii inazidi kuwa na msisimko mkubwa nchini tunawashukuru wadau  wote na tuna imani kuwa itazidi kuwa bora katika siku za usoni

Alisema kuwa Vodacom Tanzania itaendelea kutoa udhamini wa ligi hii hata katika msimu ujao kwa mujibu wa mkataba wake na TFF na aliwataka wadhamini wengine kujitokeza ili kuboresha zaidi ligi hii ikiwemo kuwawezesha wachezaji kunufaika zaidi katika ushiriki wake.

KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP

*********

JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU:

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: GlobalPublishers

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE: @shigongotz

Leave A Reply