The House of Favourite Newspapers

Zitto Amuomba Radhi CAG Kichere

0

KiONGOZI wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe  leo Aprili 11, amemuomba radhi mdhibiti na mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere kwa shutuma alizomrushia siku za nyuma, akibainisha kuwa kipindi hicho Kichere alimtuma mmoja wa wabunge amueleze Zitto kuwa anafanya kazi kwa mujibu wa taratibu na si vinginevyo.

 

Kipindi kile nilitoa maneno makali kidogo kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali huyu wa sasa Bw. Charles Kichere na kusema kwamba ni mtu ambaye ameteuliwa ili kwenda kulinda maslahi ya serikali na watu wake” Zitto Kabwe.

 

“Alimtuma mmoja wa waliokuwa wabunge wenzangu wakati ule kutoka mkoa wa Kigoma aje kuniambia kwamba nimwamini yeye ni Proffesional, atafanya kazi yake kwa weledi asubiri nione nisimuhukumu, hakika ameni-Prove Wrong kwa ripoti yake ya mwaka huu” Zitto Kabwe.

 

“Ameonyesha kwamba hasira zangu za wakati ule dhidi yake zilikuwa “misplaced” na ninamuomba radhi ilikuwa ni hasira za kutaka katiba ilindwe na ameonyesha kwa vitendo anafanya kazi yake kwa weledi” Zitto Kabwe.

 

 

Leave A Reply