The House of Favourite Newspapers

Zlatan Ibrahimovic Ashtakiwa Uingereza

Mshambuliaji wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic na Mlinzi wa Bournemouth Tyrone Mings wote wawili wameshitakiwa na chama cha soka nchini Uingereza FA, kwa makosa ya kinidhamu.

Wachezaji hao waligombana kwenye mchezo wa ligi ya kuu nchini England (EPL), baina ya timu zao, ulioisha kwa sare ya 1-1, Jumamosi iliyopita, wakati Mings, 23, alipomkanyaga kichwani Ibrahimovic, kisha baadaye naye Ibrahimovic akajibu kwa kumpiga kiwiko Mings, wakati wa mpira wa kona.

Taarifa ya FA imesema wachezaji hao, wanapashwa kuwasilisha utetezi hao, hadi kesho saa mbili usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

“Wachezaji walihusika kwenye matukio mawili ya wakati tofauti, ndani ya dakika 44 au nje ya hapo, kitendo ambacho hakikuonekana na maafisa wa mchezo, ndani ya muda husika lakini kilibainika kwenye Video,” Taarifa ya FA, ilisema.

Vitendo vya makusudi vya wachezaji hao, vinastahili kadi nyekundu na kufungiwa mechi tatu, hivyo Ibrahimovic au Mings wote wanaweza kufungiwa wakipatikana na hatia.

Ibrahimovic anaweza kukosa mchezo wa robo fainali ya kombe la FA, dhidi ya Chelsea na michezo ya ligi dhidi ya Middlesbrough na West Brom.

Comments are closed.