The House of Favourite Newspapers

Mnaigeria Kuipa Shavu Bongo Muvi

Mike Ezuruonye

MSANII wa Filamu kutoka Nigeria, Mike Ezuruonye, ‘Mikezuu’ jana alipokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ziara ya kikazi.

Mike Ezuruonye

Mike amefunguka kuwa yupo nchini kikazi kuimalizia moja ya filamu aliyoshirikiana na wasanii wa hapa Bongo. Akipokelewa na mastaa wa filamu kibao wakiongozwa na Halima Yahya, ‘Davina’

Davina wa kwanza (Kulia) mama Kanumba (Kushoto) na mdau wa filamu wakiwa Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere

“Nimefurahi sana kumuona Mike nchini Tanzania, karibu sana Mike pia mheshimiwa waziri samahani huwa tunatumia jina lako wakati wa kuomba vibali. Kazi hii ni kubwa na tunafanya hivi ili kuipanua soko la filamu nchini,” alisema Davina

Aidha Waziri wa Sanaa na Michezo Nape Nauye, alikuwepo uwanjani hapo.

Salum Milongo/GPL

Comments are closed.