The House of Favourite Newspapers

Zlatan Ibrahimovic I’m Back!!

0
Zlatan Ibrahimovic

WAKATI leo saa 8:30 mchana Manchester United itaivaa Tottenham Hotspur katika Ligi Kuu England, Zlatan Ibrahimovic amesema; “Narudi, kuanzia pale nilipoishia.”

 

Zlatan amesema atarejea uwanjani Desemba mwaka huu akitoka katika majeraha ya muda mrefu ya goti.

Straika huyo akiichezea Man United katika msimu wake wa kwanza msimu uliopita, aliisaidia kuipa mataji ya Ngao ya Jamii, Europa League na Kombe la Ligi.

 

Hata hivyo, ndoto za Zlatan, 36, kuendelea kuitumia Man United zilififia mwishoni mwa msimu uliopita baada ya kuumia goti na kulazimika kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu.

 

Alipoumia Zlatan, mkataba wake wa mwaka mmoja ulikuwa ukieleekea kuisha na akaomba asilipwe sehemu ya mishahara yake iliyobaki lakini Kocha Jose Mourinho alimshawishi akaongeza mkataba mwingine wa mwaka mmoja.

 

“Nimerudi kumalizia sehemu nilipoishia,” alisema Zlatan ambaye msimu uliopita aliifungia Man United mabao 28 katika michuano yote.

“Tayari nina mataji matatu na klabu hii, mwisho wangu si mwisho wa kile tunach-ohitaji, narudi uwanjani huku lengo kuu likiwa ni kutwaa ubingwa wa Premier League.”

 

Leo, Man United inaikaribisha Spurs kwenye Uwanja wa Old Trafford kucheza mechi ya Ligi Kuu England, mchezo unaotajwa kuwa mkali na wa kuvutia.

Man United ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 20 sawa na Spurs iliyo katika nafasi ya tatu.

Leave A Reply