The House of Favourite Newspapers
gunners X

Zuchu Aja na Home Coming Show – Video

0

MREMBO kutoka Wasafi Classic Baby (WCB), Zuhura Othuman ‘Zuchu’ anatarajia kufanya shoo kubwa maarufu kwa jina la Home Coming pande za Zanzibar, Agosti 21, 2021.

Zuchu amefunguka hayo leo kwenye mkutano wa waandishi wa habari alipokuwa akielezea maandalizi ya shoo hiyo ambapo amesema, itakuwa shoo itakayowakutanisha wasanii wengi kutoka visiwani humo.

Amesema amepata wazo hilo na ameona ni wakati sahihi wa yeye kurudi nyumbani, kufanya jambo kubwa na wasanii wenzake hivyo mashabiki wa burudani waendelee kufuatilia mitandao yake ya kijamii pamoja na vyombo vya habari ili kupata orodha kamili ya wasanii watakaopafomu.

Mbali na shoo hiyo, Zuchu amesema kutakuwa na semina mbalimbali maalum kabla ya shoo itakayolenga kuwajengea uelewa wasanii hususan wa Zanzibar katika suala zima la kujitangaza kupitia mitandao ya kijamii na masuala mengine mengi yanayohusu sanaa.

Written by @erick.evarist cc @hotpot_tz

 

Leave A Reply