The House of Favourite Newspapers

Acb Yaendelea Kutoa Mbinu Za Mafanikio Kwenye Vicoba

0
Meneja Masoko wa Benki ya ACB, Innocent Ishengoma akizungumza na umati uliofurika kwenye uzinduzi huo.

Benki ya Akiba Commencial (ACB) jana iliungana na kikundi cha vicoba cha TEYOTA katika uzinduzi wa kikundi hicho uliofanyika jana katika Baa ya Abiola iliyopo Yombo Buza Temeke, Dar na kuwapa somo na la mafanikio ya fedha wanakundi hao.

 

Katika uzinduzi huo uliambatana na burudani mbalimbali, Meneja Masoko wa Benki hiyo, Innocent Ishengoma amewataka wanachama kikundi kuwa ni nidhamu ya fedha ili kufikia malengo yao ya uwekezaji.

Akizungumzia malengo hayo aliwaambia wanachama hao kuwa benki yake imeanzisha akaunti malengo iitwayo Akiba LIP.

Walimu wa kufundisha elimu ya vicoba wakiwa kwenye uzinduzi huo.

LIP ni akaunti ya malengo ambayo mwanachama atajiwekea pesa na kujipangia siku yake ya malengo kuichukua pesa hiyo.

Wafanyakazi wa ACB (wenye fulana nyeusi) wakimsaidia mmoja wa wanachama wa vicoba kufungua akaunti ya malengo (LIP).

Ishengoma amesema akaunti itamuwezesha muwekaji kuweza kutimiza malengo mbalimbali ikiwemo kulipa ada, kununua kiwanja, gari, mtaji wa biashara na mambo mengine mengi.

 

Baada ya kuelemishwa juu ya akaunti hiyo umati wa wanachama uliofurika kwenye uzinduzi huo walionekana kufungua akaunti hiyo.

HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS GPL

Leave A Reply