The House of Favourite Newspapers

Ajali ya basi na lori yaua 11 Tanga

0

ajali ya basi na lori (1)

WATU 11 wamepoteza maisha  huku 29 wakijeruhiwa baada ya basi la abiria la Simba Mtoto lililokuwa linakuja jijini Dar es Salaam kupata ajali kwa kugongana na lori katika kijiji cha Pangamlima, Barabara ya Tanga-Segera mkoani Tanga leo asubuhi. Miongoni mwa waliopoteza maisha ni madereva wawili wa lori na basi.

ajali ya basi na lori (2)

Tovuti hii imeongea na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Mihayo Msikhela ambaye amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza kuwa kwa taarifa za awali chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa lori ambaye alikosa umakini baada ya kusinzia huku akiendesha.

ajali ya basi na lori (3)

Leave A Reply