The House of Favourite Newspapers

Ajifungua Mapacha Wenye Vichwa Viwili, Miguu Mitatu

0

MWANAMKE mmoja ka­tika mji wa Parkinson nchini India amejifungua mapacha adimu duniani walioun­gana ambao wana vich­wa viwili, mwili mmoja na mikono mitatu.

Babita Ahirwar (21) na mumewe Jaswant Singh waliambiwa na madaktari wakati wakihudhuria kliniki kuwa wangepata watoto mapacha.

 

Hata hivyo wiki ya 34 ya ujauzito, madaktari waliokuwa wakimhudumia Babita waligundua kitu cha tofauti kuwa mapacha hao hawakuwa wa kawaida.

“Mke wangu aliumia baada ya kumwona mtoto wetu na kusema kweli, tumesh-tushwa.

“Kila mtu anashtuka kuwaona. Hatuwezi kuamini mtoto wetu ana vichwa viwili. “Tuliambiwa baada ya uchunguzi wa kitabibu kuwa tutakuwa na mapacha. Tulifurahi sana kupata watoto wawili lakini ni mtoto mmoja mwenye vichwa viwili.

 

“Basi tena, huyu ni mtoto wangu na nitamlea, watu wanasema mambo mengi lakini yeye ni mtoto wangu na nitampeleka nyumbani.

“Sina pesa ya kumfanyia operesheni. Maadamu yuko hai, nitampenda na kumjali,” alisema Jaswant.

Naye mtaalam wa watoto katika hospitali ya wilaya mjini humo, Dk Surendra Sonkar alisema, mtoto huyo ni wa aina yake na kwamba atahamishiwa kwenye kitengo cha hali ya juu kwa matibabu.

 

“Ni kesi ya mapacha adimu, tumezoea kuona mapacha wanaoji-tegemea viungo hasa vya ndani lakini huyu viungo vyake muhimu vimeungana.

“Tunamtunza mtoto na tutachukua maoni ya madaktari huko Bhopal na Delhi,” alisema Dk Surendra.

MWANDISHI WETU NA MTANDAO

Leave A Reply