The House of Favourite Newspapers

Muna Awatolea Uvivu Mashabiki

0

MSANII wa kitambo kwenye tasnia ya filamu Bongo, Rose Alphonce ‘Muna Love’ amesema hata watu wakimsema kiasi gani, kamwe hawezi kubadilika kwenye mavazi yake au kuweka nywele anazopenda kichwani kisa kuokoka.

 

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Muna amesema kuwa watu wanafikra za kizamani kwamba ukiwa mlokole basi usipendeze kwa chochote na kichwani kuvaa kitambaa wakati wote, kitu ambacho yeye anakipinga.

 

“Jamani nywele niweke rangi zozote kuna shida gani? Kinachotakiwa ni kumjua Mungu wako unayemtumikia na wala hataki kabisa kumuona mtu hajipendi na hata kufika kwako itakuwa ngumu sana kama utakuwa mchafu na usiyenukia kiusafi,” alisema Muna ambaye kwa sasa ameokoka na kufanya shughuli nyingi zaidi za kidini.

Leave A Reply