The House of Favourite Newspapers

AUNT AKATA NGEBE ZA UWOYA

DAR ES SALAAM: Staa mkubwa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel amefanya kufuru kubwa na kumfunika staa mwenzake, Irene Uwoya baada ya kufungua pub yake kubwa ya kisasa iliyopo Mikocheni, jijini Dar, maeneo ya Kwa Ridhiwani ambayo anatarajia kuizindua leo.  Aunt anafungua pub hiyo ya kisasa ikiwa ni baada ya kupita kipindi kirefu tangu Uwoya afungue pub yake maeneo ya Sinza-Mori jijini Dar inayofahamika kwa jina la Last Munities.

Kwenye pub hiyo ya Aunt ambayo ameipa jina ya The Luxe, ina sehemu kubwa ya kupumzikia kwa nje wakati ukipata vinywaji lakini pia kuna sehemu ya ndani ya kupumzikia. Kama hiyo haitoshi, kwenye pub hiyo kuna sehemu ya kupata vinywaji na chakula zenye mandhari tofauti ambazo zinaweza kumvutia mteja kulingana na matakwa yake.

Pamoja na maeneo hayo ya kupata chakula pamoja na vinywaji, kuna chumba maalum cha masaji hivyo kama mteja atakuwa amechoka na starehe anaweza kuingia ndani na kupata huduma hiyo. Amani lililofika kwenye pub hiyo pia lilishuhudia sehemu maalum kwa ajili ya chakula kukiwa na mpishi hodari ambaye atakuwa akipika vyakula vya kila aina kwa ajili ya wateja wake. Baadhi ya watu waliozungumza na Amani baada ya kuiona pub hiyo, walisema imewashtua kwani hawakutegemea kama Aunt naye anaweza kuwa na kitu kikubwa namna hiyo.

“Mh! Imetushtua kwa kweli sisi kama mashabiki wake lakini kwa kweli tunampongeza,” alisema Jenifa Kilamba, mkazi wa Mikocheni Dar.Amani liliweza pia kuzungumza na Aunt ambapo alipoulizwa kuhusu gharama alizotumia kupanga na kuijenga pub hiyo, hakuwa wazi kuzianika. Aunt alisema kuwa ni mapema sana kuzungumzia gharama lakini ieleweke tu kwamba ametumia fedha nyingi.

“Ninamshukuru Mungu kukamilisha hili kwa kweli sio kazi ndogo hata kidogo, na nimetumia hela nyingi ili nitengeneze kitu kizuri na bado siko tayari kusema gharama kwa sasa ila ieleweke tu ni nyingi sana,” alisema Aunt. Warembo wa Bongo Movies kwa sasa wanaonekana kujikita kwenye ujasiriamali ambapo mbali na Aunt na Uwoya, wapo Zuwena Mohamed ‘Shilole’ anayemiliki mgahawa na Wema Sepetu (duka la nguo).

Comments are closed.