VIDEO: TCRA Yatoa TAMKO Yanayotokea MITANDAONI

Waziri wa Ujenzi na Mawasiliano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Sira Ubwa ameipongeza mamlaka ya Mawasilino nchini TCRA kwa kuboreshaji huduma wanazotoa ili kutimiza azma ya Serikali yenye lengo la kuboresha sekta ya mawasilaino nchini.

Waziri Ubwa ameyasema hayo hii leo wakati alipofanya ziara maalumu ya kikazi kujionea mifumo ya utendaji kazi ya taasisi hiyo katika makao makuu yake yaliyopo eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi nchini Atashasta Nditiye ameitaka mamalaka hiyo kufuatilia na kuchukua hatua dhidi ya kampuni za mawasiliano zinazokiuka maeleekezo ya Serikali juu muongozo wa watumiaji wa mawasiliano uliopangwa kuanza utekelezaji wake Januri 2019.

Mamlaka ya mawasiliano Tanzania ilinzishwa kwa sheria ya uthibiti mawasiliano namba 12 ya mwaka 2003 ikiwa na lengo la kusimamia na kuthibiti mifumo ya mawasiliano ya kielectronik na posta hapa nchini.


Loading...

Toa comment