The House of Favourite Newspapers

Basi lagongana na lori na kuua watu Singida

BREAKINGNEWS3 ajali basi

basi (1) basi (2) basi (3)

WATU 12 wamekufa papo hapo na wengine 18 kujeruhiwa baada ya basi la Kampuni ya Taqbir kugongana na lori la mafuta mkoani Singida.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Thobias Sedoyeka amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema basi lilikuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Katoro mkoani Geita.

Ajali hiyo imetokea leo saa 1:30 usiku katika eneo la Kizonzo, Wilaya ya Iramba mkoani Singida ikilihusisha basi aina ya Scania lenye namba za usajili T 230 BRJ lililokuwa likiendeshwa na Charles Kikaena lililogongana na lori la mafuta T 793 CBH lililokuwa na tela T 273 CBH lilokuwa likiendeshwa na dereva Mohamed Rajabu.

Chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa basi aliyekuwa akilipita lori mali ya kampuni ya Coca Cola lenye namba T 314 CTS lililokuwa na tela T 196 BEF na kugongana na lori la mafuta na kisha lori hilo kulichana basi kuanzia mbele upande wa dereva hadi mwisho na kusababisha vifo hivyo vya watu 12 na majeruhi 18 na basi hilo lilikuwa na abiria 51.

Miongoni mwa waliokufa ni wanaume saba akiwemo mtoto mdogo mmoja na wanawake watano kati yao watoto wawili.

Majeruhi wa ajali hiyo walifikishwa katika Hospitali ya serikali ya Kiomboi mkoani Singida kwa matibabu.

Comments are closed.