The House of Favourite Newspapers

Championi Yawaibukia Tena ‘Vibandaumiza’ Dar

0

1   Ofisa Masoko wa Kampuni ya Global Publishers, Yohana Mkanda (kushoto) akimkabidhi Salum Magoma, Mkazi wa Kinondoni Makuti ubao wa kuandikia ratiba za kuonesha mpira.

2Mkanda akimkabidhi ubao wa kuandikia ratiba za kuonesha mpira, Shukuru Bantu, Mkazi wa Kinondoni-Hananasifu.

3Fadhiri Juma (kulia), akikabidhiwa ubao na Mkanda.

4Ode Singa (kulia), Mkazi wa Ilala-Sharifu Shamba akikabidhiwa ubao wake na Mkanda.

5Samson Henry (kulia), mkazi wa Buguruni Malapa akikabidhiwa ubao wake.

6Nicholaus Lucas (kulia), Mkazi wa Tandika Mwisho akikabidhiwa ubao wake na Mkanda.

7Issa Dokta (kulia), Mkazi wa Magomeni-Mwembe Chai Dar akikabidhiwa ubao wake na Mkanda.

8Juma Arteta (kulia), naye akipokea ubao wenye Nembo ya Gazeti la Championi.

9Mnubi Junior (kulia),  Mkazi wa Magomeni akikabidhiwa ubao wake na Mkanda.

GAZETI namba moja la michezo Tanzania la Championi, leo limegawa mbao za matangazo kwa mara ya pili baadhi ya sehemu za kuoneshea mpira maarufu kama vibanda umiza vilivyopo maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar.

Zoezi hilo la ugawaji wa mbao hizo limefanywa kwa nia ya kulitangaza gazeti hilo linalomilikiwa na Kampuni ya Global Publishers Ltd na kuwajali wapenzi wasoka nchini, ambapo ofisa masoko wa kampuni hiyo, Yohana Mkanda alizunguka maeneo mbalimbali yakiwemo Mkwajuni, Magomeni Mwembe Chai, Ilala-Bungoni, na Tandika ambapo wenye vibanda walinufaika na mbao hizo.

“Lengo letu ni kuimarisha uhusiano kati yetu na mashabiki wa soka ambao ndiyo wadau wakubwa wa Gazeti la Championi, tutaendelea kuzunguka sehemu nyingine nyingi kugawa mbao hizo,” alisema Mkanda.

Na Denis Mtima/GPL

Leave A Reply