The House of Favourite Newspapers

Watanzania Waifagilia Intaneti ya 4G ya Vodacom

0

4 G

MAPINDUZI katika teknolojia yaliyofanywa na Kampuni ya Vodacom Tanzania kwa kuanza kutoa huduma ya intaneti yenye kasi kubwa ya 4G umepokelewa vizuri na Watanzania ambao ni watumiaji wa huduma za intaneti jijini Dar es Salaam.

Wateja ambao ni watumiaji wa siku nyingi wa intaneti walipohojiwa na www.globalpublishers.co.tz walisema kuwa awali walikuwa wakitumia intaneti ya mitandano mingine lakini baada ya kuanza kuitumia 4G ya Vodacom wameona kuna utofauti mkubwa kwani imekuwa na kasi zaidi.

Walisema kuwa huduma hii imekuwa ikiwarahisishia kwenye kazi zao mbalimbali za kila siku kwani wanapo ‘download’ au ‘ku-upload’ imekuwa ikiwachuku muda mfupi tu kukamilisha kazi hiyo.

Mmoja wa watumiaji hao ni, Hamis Hassan mkazi wa Manzese alisema; “Kwa kweli hii intaneti ya 4G ya Vodacom ndiyo habari ya town, yaani walipozindua huduma hii tu, na mimi fasta nikaanza kuitumia, kila nikiilinganisha na ile niliyokuwa naitumia zamani kwa kweli kuna tofauti kubwa sana, huku nilipo nateleza tu iko fasta kweli.”

Naye Imelda Justus wa Sinza alisema; “Kwa muda mrefu nilikuwa nahangaika na mitandao mbalimbali, nimebadili sana modem, lakini bado tatizo la intaneti sikulitatua mpaka majuzi nilipoanza kutumia 4G ya Vodacom kila jambo limebadilika na kwa sasa nainjoi na intaneti yenye kasi ya ukweli.”

Intaneti ya 4G ya Vodacom Tanzania inamuwezesha mtumiaji wa mawasiliano ya simu kuperuzi kurasa za mitandao, kutuma na kupokea picha na video kwa haraka na kupakua nyaraka mbalimbali na picha kutoka kwenye tovuti mbalimbali kwa kasi kubwa.

Ili kufurahia huduma hii, mteja wa Vodacom anapaswa kuwa na kadi ya simu ya Vodacom 4G pamoja na simu iliyowezeshwa kutumia teknolojia ya 4G ambavyo vyote hivyo vinapatikana kwa urahisi kutoka katika maduka yote ya Vodacom jijini Dar es Salaam.

Leave A Reply