The House of Favourite Newspapers

Fedha za Kessy zasajili Yanga Yote!

0

Kessy

Beki wa timu ya Yanga, Hassan Kessy.

Mwandishi Wetu,
Dar es Salaam
HAKIKA hii ni kali ya mwaka! Baada ya mzunguko mrefu hatimaye Simba wamewaonyesha Yanga kufuru baada ya kutaka timu hiyo iwalipe shilingi bilioni moja na milioni mia tatu, kwa ajili ya kumpata beki .

Kessy, alisajiliwa na Yanga kwenye usajili huu wa Ligi Kuu Bara akitokea Simba kwenye usajili ambao umejaa utata mkubwa, hata hivyo, ameshaichezea timu hiyo michezo mitatu ya kimashindano, lakini bado figisu ni ya hali ya juu.

 
Klabu ya Simba imetinga kwenye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kuwasilisha hoja ya kuitaka Yanga kuwapa fedha ndefu ambazo zipo katika kipengele cha mkataba baina ya mchezaji huyo na klabu hiyo endapo upande mmoja utauvunja.
Kessy aliondoka Simba na kutua Yanga katika dirisha la usajili lililofungwa Agosti 6, mwaka huu ambapo beki huyo aliondoka huku akiwa na migogoro na viongozi wa timu hiyo ambao walimfungia kuichezea timu hiyo mechi tano kutokana na kumchezea vibaya aliyekuwa straika wa Toto African, Edward Christopher.

KESSY (2)

 

Akifunga kamba a viatu.

Habari za ndani kabisa ambazo Championi Jumatano limezipata kutoka katika mmoja wa vigogo wa Simba ni kwamba timu hiyo imewasilisha hoja hiyo kwa kumtaka Kessy kuwalipa kwa kitendo chake cha kuanza kuitumikia Yanga kabla mkataba wake haujaisha, alipotinga Uwanja wa Taifa, Dar katika fainali ya Kombe la Shirikisho (FA) Mei 25, mwaka huu wakati mkataba wake ukiwa unaisha, Juni 15.
“Awali Simba waliwaambia Yanga wawalipe dola 60,000, ili kumaliza ishu hiyo kishkaji lakini wao kwa upande wao hawakutoa fedha hizo, hivyo sasa viongozi wa Simba wameamua kufuata suala hilo kisheria ambapo wamepeleka barua TFF ya kumtaka beki huyo kuilipa timu fidia ya dola laki sita (600,000) ambazo ni sawa na shilingi bilioni 1.3, ikiwa ni sehemu ya kuvunja mkataba wake kama ulivyoainishwa.

 

“Unajua mkataba wa Kessy na Simba ulikuwa na kipengele kinasema kwamba endapo beki huyo atavunja mkataba huo ni lazima ailipe klabu hiyo fedha hizo sasa walipowaambia Yanga wenyewe waliwapuuzia, ndiyo maana muda huu wameenda kisheria zaidi.
“Lakini kingine ambacho viongozi wa Simba wameamua kuchukua maamuzi hayo ni kutokana na beki huyo kuvunja mkataba kwa kuanza kujihusisha na Yanga wakati akiwa anatambua wazi ana mkataba na timu hiyo ambao ulikuwa unamalizika Juni 15 lakini yeye alianza kuonekana na jezi za Yanga tangu Mei 25, mwaka huu,” alisema kigogo huyo.
Kwa uhakika ambao Championi inao ni kwamba kama Yanga watatoa kiwango hicho cha fedha, kwanza itakuwa ni kufuru kwa fedha hiyo kuwahi kutolewa kwenye usajili Tanzania, lakini pia itakuwa rekodi kwa kuwa zinaweza kusajili Yanga nzima na chenji inabaki.

KESSY (3)

Kwenye kikosi cha Yanga cha sasa, mchezaji aliyesajiliwa ghali zaidi, yupo kwenye benchi ambaye ni Obrey Chirwa, aliyesajiliwa kwa kitita cha jumla ya shilingi milioni 240.
Mchanganuo mzima unaonyesha kuwa kikosi cha kwanza cha Yanga kina jumla ya shilingi milioni 540, huku Vincent Bossou na Donald Ngoma wakiwa wanabeba figa hiyo kwa kila mmoja kusajiliwa kwa milioni 100.

 

Kwa upande wa benchi kuna wachezaji saba ambao wana jumla ya shilingi milioni 470, ambazo ukijumlisha na zile za kikosi cha kwanza utapata jumla ya shilingi bilioni moja na milioni 10.
Hii ina maana kuwa ukichukua bilioni moja na milioni mia tatu ambazo Simba inamdai Kessy, ukitoa shilingi bilioni moja na milioni kumi, utabaki na shilingi milioni 290, ambayo ndiyo chenji.
Angalizo, fedha hizi ni zile ambazo Championi lilizipata wakati wachezaji hawa wanasajiliwa na timu hiyo ya Jangwani au waliposaini mikataba mipya na timu hiyo.
Mchanganuo kamili wa fedha za usajili Yanga ni kama ifuatavyo:

Kikosi cha kwanza:
Deogratius Munish ‘Dida’ : Mil 30
Juma Abdul: Mil 30
Mwinyi Haji: Mil 20
Andrew Vincent ‘Dante’: Mil 35
Vincent Bossou: Mil 100
Thabani Kamusoko: Mil 70
Simon Msuva: Mil 50
Haruna Niyonzima: Mil 70
Amissi Tambwe: Mil 50
Donald Ngoma: Mil 100
Deus Kaseke: Mil 35

Waliopo benchi
Benno Kakolanya: Mil 30
Hassan Kessy: Mil 40
Obrey Chirwa: Mil 240
Mbuyu Twite: Mil 35
Kelvin Yondani: Mil 60
Juma Mahadhi: Mil 35
Oscar Joshua: Mil 30

Leave A Reply