The House of Favourite Newspapers

Kadja Nito azidi kuteswa na menejimenti

0

Nito

MREMBO anayesumbua kunako gemu la Muziki wa Bongo Fleva, Khadija Maige ‘Kadja Nito’ ambaye kwa sasa anatamba na ngoma iitwayo One More Nigt aliyofanya na Yogo Beats huku kichupa kikishutiwa na GQ Digital Vibes, amesema kuwa tatizo kubwa linalozidi kumtafuna hata asiweze kusimama vizuri kikazi ni kukosa menejimenti.

Akipiga stori na safu hii ya burudani, mrembo huyo alisema amejitahidi kutafuta menejimenti kwa nguvu nyingi lakini bado jitihada zake zimegonga mwamba jambo linalomuumiza wakati mwingine kwa sababu anakutana na changamoto nyingi za kikazi ambazo zingine anashindwa kuzitatua peke yake.

“Suala la kukosa menejimenti linanitesa sana, nimekwisha shika soko la nyumbani kwa sasa kwa kiasi fulani ambapo nilikuwa nataka kutanua wigo wangu wa mashabiki kwa kufanya kazi zenye ubora zaidi lakini nashindwa kwa sababu tu sina menejimenti ya kunisapoti kufanya kazi hizo na kuwafikia watu wengi ambao wengine wako nje ya nchi,” alisema Khadja Nito.

 

Leave A Reply