The House of Favourite Newspapers

Aua wawili, asakwa

0

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Zuberi MwombejiStori: STEPHANO MANGO, Risasi Jumamosi

SONGEA: JESHI la Polisi mkoani Ruvuma linamsaka dereva wa daladala inayofanya safari zake kati ya Songea na Peramiho kwa kosa la kuwaua watu wawili baada ya kuwagonga na gari na kutokomea kusikojulikana, tukio lililotokea wiki iliyopita katika eneo la Mkomi, katika barabara ya kuelekea Mbinga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Zuberi Mwombeji (pichani) alisema dereva huyo alianza kwa kumgonga na kumuua mwendesha bodaboda kabla ya kuyumba na kupoteza mwelekeo uliosababisha kumparamia mwenda kwa miguu na kumpotezea maisha yake papo hapo.

Alimtaja mwendesha bodaboda aliyefariki dunia kuwa ni Frank Mahundi (18) mkazi wa Lizaboni Manispaa ya Songea na mtembea kwa miguu ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja, lakini umri wake ukikadiriwa kuwa kati ya miaka 20-25.

Dereva huyo aliyekuwa akiendesha gari aina ya Nissan Caravan yenye namba za usajili T 811 AHG hajulikani alipo, lakini kamanda huyo amesema juhudi za kumtafuta zinaendelea. Mwili wa Mahundi ulichukuliwa na ndugu zake wakati ule wa mtembea kwa miguu ambaye bado hajatambuliwa, ukiwa umehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma.

Leave A Reply