The House of Favourite Newspapers

Khadija Kopa Kuwasha Moto Krismas Morogoro (Picha&Video)

khadija-kopa-1

Mwenyekiti na mratibu wa tamasha hilo, Hamis Abdallah,  akizungumza jambo na wanahari (hawapo pichani).

khadija-kopa-2

Kutoka kushoto ni mkuu wa matukio kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Kurugira Maregesi,  Hamis Abdallah na Khadija Kopa.

khadija-kopa-3

Khadija Kopa akizungumza jambo.

khadija-kopa-4

Kiongozi wa FM Academia, Nyoshi El Saadat, akielezea namna atakavyopagawisha mashabiki wake.

MALKIA wa muziki wa taarab ambaye ni Mkurugenzi wa Kundi la Ogopa Kopa, Khadija Kopa,  anatarajiwa kuwasha moto kwa kutoa burudani ya aina yake katika  Tamasha la Muziki wa Taarab  lililoandaliwa na mtandao wa habari wa Vijana, Tegemeo Arts Group ambalo linajulikana kwa jina la ‘Nani Zaidi’.

Tamasha hilo litakaofanyika siku ya X-Mass ya Desemba 25 mwaka huu kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro kuanzia saa nne asubuhi mpaka saa kumi usiku.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, mwenyekiti na mratibu wa tamasha hilo, Hamis Abdallah,  amesema tamsha hilo linalenga kuhamasisha jamiii katika uchangiaji wa damu ili kuokoa maisha kwa wenye uhitaji hasa kina mama wanapopoteza maisha kwa kutokwa na damu nyingi wakati wa kujifungua.

Amesema kwamba katika zoezi hilo pia kutakuwa na upimaji wa Ukimwi , saratani ya mlango wa kizazi kwa wanawake na kutakuwa na maonyesho ya bidhaa mablimbali siku tano kabla ya tamasha hilo.

 

Alifafanua kuwa tamasha hilo litakuwa la aina yake kwani litakutanisha bendi za muziki wa dansi na wanamuziki wa taarab chini.

Miongoni mwa makundi ya taarab na bendi zitakazokuwepo ni Jahazi Modern Taarab, Ogopa Copa Clasic Band,  The East African Melody,  Five Stars Modern Taarab, FM Academia na Moro Jazz.

Mbali na hayo pia  kutakuwa na mechi katika ya Tanzania Veterans na Morogoro Veterans zote za mjini Morogoro zitakazokipiga Desemba 24 mwaka huu zikilenga kuhamasisha uchangiaji hiari wa damu.

Na Denis Mtima/GPL

Comments are closed.