The House of Favourite Newspapers

Covenant Bank Yakipiga Jeki Kijiji cha Kituri, Mwanga

1

Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Mathabetha Mwambenja (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi ya milioni tano na laki mbili mwakilishi kutoka Kijiji cha Kituri Mkoa wa Kilimanjaro, Amin Salim.

2

…Akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).

3

Mwakilishi wa kijiji cha Kituri, Amini Salim (kushoto) akizungumza jambo.

Covenant Bank jijini Dar es Salaam leo imekipiga jeki kijiji cha Kituri cha Wilaya ya Mwanga, Kilimanjaro, kwa kukikabidhi hundi ya shilingi milioni tano na laki mbili.

Akizungumza katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar, Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Mathabetha Mwambenja, alisema kuwa wao wameguswa na suala zima la kijamii na hivyo kuiwezesha zahanati hiyo inayojengwa kijiji cha Kituri kiasi cha fedha hizo ili ziweze kuimarisha miundombinu ya umeme katika zahanati hiyo.

Naye mwakilishi kutoka katika kijiji hicho aliyefika jijini Dar kwa ajili ya kupokea msaada huo, Amin Salim, aliishukuru benki hiyo akiwaomba waendelee na moyo huo.

Na Hilaly Daudi/GPL

Comments are closed.