The House of Favourite Newspapers

Machangu: Tunahamia Dodoma

0

machangu (4)Madada poawakijiuza.

Na Waandishi Wetu, AMANI

DAR ES SALAAM: ”Kama serikali yote inahamia Dodoma kwenye makao makuu ya nchi, ina maana hapa Dar hakutakuwa na maana tena! Wateja wote ni Dodoma sasa sisi tunasubiri nini? Na sisi tunahamia Dodoma,” ndivyo alivyosikika dadapoa mmoja aliyegoma kutaja jina lake, lakini kijiwe chake kikiwa maeneo ya Sinza Afrikasana, Dar.

machangu (3)Wiki hii, Amani liliamua kufanya mahojiano na uchunguzi kwa machangudoa wa maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Kinondoni kuwasikia wanasemaje kuhusu tamko la serikali kuwa, wizara zote zinahamia Dodoma ambako ndiko kwenye makao makuu ya serikali.

Amani liliamua kuzungumza na akinadada poa hao baada ya kuwepo madai kwamba, mji wa Dodoma umeanza kupokea wageni kutoka nje ya mkoa huo ambao wamekwenda kusaka fursa mbalimbali kutokana na serikali kuhamia huko.

machangu (2)WASIKIE HAWA

Baadhi ya machungudoa wa eneo hilo la Afrikasana walisema kuwa, baada ya kuona wimbi la watu wanataja Dodoma na wao wamejipanga kuhamia huko kwa kuendeleza biashara hiyo.

“Mimi mfano, natokea Tanga, nimekuja Dar kwa ajili ya kujiuza, sasa serikali inapohamia Dodoma maana yake ni kwamba, mambo mengi, yatahamia kule. “Nimesikia watu wakisema kuwa, hapa Dar patabaki peupe kwani hata foleni zitakwisha, msongamano utakuwa Dodoma.

machangu (1)Sasa mimi Dar nabaki kufanya nini?” alisema mmoja wa machangu hao akisema anaitwa Mwajabu Idi, mkazi wa Mapinduzi, Tanga. Mwenzake aliyedai anaitwa Kidawa, mkazi wa Morogoro alisema: “Kwenda Dodoma si hiari yetu bali ni hali halisi. Kazi yetu (ya kuuza miili) haina tofauti na wafanyabiashara wengine, unaangalia soko liko wapi? Kwa hiyo kama soko litahamia Dodoma na sisi hukohuko.”

HALI YA DODOMA KWA SASA

Amani lilizungumza na baadhi ya wakazi wa Dodoma ambao walisema kuwa, tangu Rais Dk.

John Pombe Magufuli ‘JPM’ atangaze kwenye Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwamba, ndani ya miaka minne na miezi minne iliyobaki ya utawala wake, serikali yote itahamia Dodoma, mji huo umebadilika ghafla.

“Na si kwa tangazo la Magufuli tu. Hata Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipotangaza kwenye maadhimisho ya Siku ya Mashujaa, Julai 25 hapa mjini Dodoma kwamba yeye atakuwa wa kwanza kuhamia Dodoma Septemba mwaka huu, hali kwenye mji huu imebadilika.

“Baadhi ya wenye nyumba wameanza kupandisha bei ya vyumba, nyumba. Wenye viwanja nao bei juu. Lakini matajiri wenye hoteli nao wameanza kukarabati wakijua wanaingia kwenye ushindani wa kibiashara,” alisema mkazi mmoja wa mji huo aliyejitambulisha kwa jina la Msokola.

WAFANYABIASHARA WA DAR

Sambamba na hali hiyo, wafanyabiashara wengi wa jijini Dar es Salaam wameanza kujipanga kwa uwekezaji mkubwa utakaofanyika mjini Dodoma.

“Unajua awamu zote zilisema zitahamia Dodoma. Alianza Baba wa Taifa (Julius Nyerere), akaja Mzee Ruksa (Ali Hassan Mwinyi), akaja mzee Mkapa (Benjamin) na hata JK (Jakaya Kikwete).

“Lakini hakuna aliyefanikisha.

Sasa huyu JPM bwana hanaga utani wala kusubiri. Akisema amesema, najua kweli atahamia Dodoma, we utaona. Ndiyo maana hata sisi wafanyabiashara tunajipanga kwenda Dodoma,” alisema Alex Shayo, mfanyabiashara wa baa, Kimara.

Leave A Reply