The House of Favourite Newspapers

Maisha Plus East Africa 2016 Yazinduliwa kwa Kishindo

1

Maisha Plus (1)

Masoud Kipanya (katikati) akiongea na washiriki waliopita wa Maisha Plus.

Maisha Plus (2)

Mkongwe wa miondoko wa Reggae nchini, Jhiko Man (kushoto) akiwa na Vitalis Maembe (aliyeshika gitaa) wakiimba pamoja.

Maisha Plus (3)

Waanzilishi wenza wa kipindi cha Maisha plus, Kaka Bonda na David Sevuri wakifurahia jambo katika uzinduzi huo.

Maisha Plus (4)

Wawakilishi kutoka Bodi ya Filamu nchini wakifuatilia uzinduzi huo.

Maisha Plus (5)

Baadhi ya wafanyakazi wa Azam Media nao walikuwemo kushuhudia uzinduzi huo.

Maisha Plus (6)

Baadhi ya wahudhuriaji wakifuatilia uzinduzi huo.

Maisha Plus (7)

Muanzilishi wa Maisha Plus, Masoud Kipanya akifungua rasmi sherehe za uzinduzi huo.

Maisha Plus (8)

Maisha Plus (9)

Maisha Plus (10)

Maisha Plus (11)

Msanii kutoka Bagamaoyo, Vitalis Maembe akitoa burudani.

Maisha Plus (12)

Masoud Kipanya akizungumza na mshindi wa Msimu wa Kwanza wa Maisha Plus, Abdul.

Maisha Plus (13)Maisha Plus (14)Maisha Plus (15)

Masoud Kipanya akimpa nafasi ya kuongea mshindi wa msimu wa pili wa Maisha Plus, Bernick Kimiro.

Maisha Plus (16)Maisha Plus (17)Maisha Plus (18)

Mkurugenzi wa Azam Media, Tido Mhando akizungumzia Maisha Plus ya msimu mpya.

Maisha Plus (19)

Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngereza akiongea jambo na waandishi wa habari (hawapo pichani).

Maisha Plus (20)Maisha Plus (21)

USIKU wa kuamkia leo ulikuwa na faraja kwa Watanzania na wafuatiliaji wa vipindi vya maisha halisi ambapo msimu mpya wa Maisha Plus East Africa 2016 ulizinduliwa rasmi katika Ofisi za Azam zilizopo Tabata jijini Dar.

Akizungumzia uzinduzi huo, Muanzilishi wa Maisha Plus, Masoud Kipanya alisema kuwa msimu huu mpya, Maisha Plus inakuja kivingine ikiwa na kauli mbiu ya Hapa Kazi Tu!

“Tunashukuru mwaka huu kwa mara ya kwanza tutaanza kuonekana katika TV ya Azam na kauli mbiu mwaka huu ni Hapa Kazi Tu, tumeona tutumie neno hilo kwa kumuunga mkono Rais John Magufuli kwa lengo la kuhamasisha vijana wafanye kazi. Ni waambie tu Hapa Kazi Tu vijana watafurahi lakini wakiingia huko kambini itakuwa Hapa Tabu Tu,” alisema Masoud.

Naye Mkurugenzi wa Azam Media, Tido Mhando alisema kuwa wamejipanga kutoa burudani ya tofauti.

“Tutakuwa na nchi kama Burundi, Rwanda na nyinginezo ambazo ni majirani zetu na zote hizo watatoa washiriki wanne kila moja hivyo kwa nchi za jirani tutakuwa na washiriki 16 na hapa Tanzania tutakuwa na washiriki 14 jumla watakuwa 30 ambapo Julai tutaanza rasmi.

“Ratiba itakuwa kuanzia Jumapili hii (Juni 5) ambapo kuanzia saa tatu usiku kupitia Azam Two tutaanza kurusha vipindi vya Maisha Plus vilipoanzia kwa kutumia teknolojia ya kisasa,” alisema Tido.

Baada ya uzinduzi huo, Maisha Plus itaanza safari za mikoni kuwapata washiriki kisha Julai wataingia rasmi kambini.

STORI/PICHA NA ANDREW CARLOS/GPL

1 Comment
  1. hafidha mussa shaaban says

    Asalam aleykoum. ..hongereni sana kwa uzinduzi wa maisha plus kwa east Africa sasa wigo wa talent utapatikana kwa vijana wote.na k ujenga udugu kwa waana wa Africa..Napenda sana haya maisha plus kwa sasa kuna vigezo vipi vya kushiriki?

Leave A Reply