The House of Favourite Newspapers

Sirro Atinga Mtaani Kutoa Elimu ya Ulinzi na Usalama

0

Sirro   Kamishna wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro akizungumza na wanachi wa maeneo ya Manzese, wakati akitoa elimu ya Ulinzi na Usalama Jijini.

Sirro2Kamanda Sirro akiendelea kutoa somo kwa wakazi wa Manzese, Dar.

Sirro3

Sirro4Sehemu ya Wananchi walioitikia wito wa Kamanda Sirro, alipokuwa akitoa somo kuimarisha ulinzi na Usalama Jijini.

Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro ameamua kuingia mtaani na kutoa elimu ya Ulinzi na Usalama Jijini huku akiwataka wananchi wanaotumia nyumba za ibada kujifunza mambo ya kivita waache mara moja maana inahatarisha amani ya nchi na kuongeza kuwa jambo hilo ‘halilipi’ hata kidogo badala yake wafanye shughuli zinazoweza kuwaingizia kipato na kuongeza uchumi wao.

Kamanda Sirro ametoa wito huo leo alipokuwa akiongea na wananchi katika katika maeneo ya Manzese, jijini Dar es Salaam ikiwa ni mwendelezo wa jitihada za kuimarisha ulinzi na usalama jijini Dar es Salaam.

(Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii)

Leave A Reply