The House of Favourite Newspapers

Mkuki Moyoni Mwangu – 43

0

KEVIN yupo New York akimtafuta mchumba wake, Catarina, ambaye amepotea katika mazingira ya kutatanisha, nyuma ya pazia, binti huyo aliyejipatia sifa katika tasnia ya mitindo, aliuawa baada ya kubakwa na tajiri Motown ndani ya ndege, kisha mpango ukafanyika na kuzikwa ndani ya Uwanja wa JF Kennedy kabla polisi hawajagundua, kwa Motown kufanya jambo hili ilikuwa ni rahisi tu sababu ya ushawishi aliokuwa nao.
FBI wameshindwa kumsaidia Kevin, hivyo basi ameamua kupeleleza mwenyewe, alipofika kwenye ofisi ya Mario Pizaro alishtushwa na kukuta tangazo kuwa Mario Pizaro alifariki dunia na mipango ya mazishi ilikuwa ikiendelea.
Kabla ya kifo cha Mario, Kevin amesikia vifo vya wafanyakazi kadhaa wa Uwanja wa Ndege wa JF Kennedy waliokufa katika mazingira ya kutatanisha, vifo vya aina moja! Moyo wake umeingiwa na hofu lakini hataki kukata tamaa, amedhamiria kuufahamu ukweli.
Je, nini kitaendelea?
SONGA NAYO…

TAARIFA za kifo cha ghafla cha Mario Pizaro zilimfanya Kevin aingiwe na hofu kubwa, hasa alipounganisha kifo hicho na cha wafanyakazi wengine wa Uwanja wa Ndege wa JF Kennedy ambao pia walikufa ghafla tena katika mtindo wa aina moja wa kifo; dawa za kulevya na kunywa pombe kali kupindukia.
“Mario hakuwa mtumiaji wa dawa za kulevya, hilo mimi nalijua!” mmoja wa majirani aliyeongea na Kevin alisema.
“Kilichotokea ni nini?”
“Hapa kuna jambo linafichwa, mimi nilikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kabisa kuingia ndani ya nyumba yake baada ya taarifa za kifo kusambazwa na mfanyakazi wake wa ndani ambaye hufanya kazi na kurejea nyumbani kwake, tulimkuta bafuni akiwa kwenye sinki la kuogea, amekufa! Kando yake kukiwa na chupa ya pombe aina ya Bond 69, kwenye mshipa wa damu bomba la sindano likining’inia, Mario ni rafiki yangu sana, hakuwahi kutumia pombe wala dawa za kulevya, nakataa! Isitoshe kitu kingine tulichokikuta bafuni kikiwa kimewekwa dirishani ni barua… naweza nikakuamini?” aliuliza jirani huyo Martin Rubio.
“Kwa nini usiniamini?”
“Subiri.” Alisema na kuondoka kuingia ndani ya nyumba yake, aliporejea alikuwa na karatasi nyeupe mkononi mwake na kumkabidhi Kevin aliyeanza kuisoma bila kupoteza wakati;
I have chosen to die because I can not keep the secret I have any longer! No one should be blamed for my death, I did it! (Nimechagua kufa kwa sababu siwezi kuendelea kuificha siri niliyonayo zaidi ya hapa, asilaumiwe mtu yeyote kwa kifo changu, nimejiua mwenyewe!)
Kevin aliisoma barua hiyo na baadaye kumwomba Martin Rubio amtolee nakala ili naye abaki nayo, mzee huyo bila kipingamizi chochote alifanya hivyo na kumpatia nakala yake, Kevin akaondoka moyoni akiwa amejawa na huzuni, machozi yakimbubujika mpaka mtaani kwake alipoishi ambako aliketi kwenye moja ya kona aliyoiita nyumbani kwake na kuanza kutafakari, moyo ukakiri kabisa maisha yake yalikuwa hatarini.
Siku iliyofuata alihudhuria mazishi ya Mario Pizaro yaliyohudhuriwa na watu wengi kwenye makaburi ya watu maarufu ya Central Cemetery katikati ya Jiji la New York, karibu kila mtu aliyejishughulisha na shughuli za urembo na mitindo duniani alikuwepo, matajiri kutoka Italia, Ufaransa na wanamitindo mbalimbali maarufu duniani walikuwepo.
Ni kwenye msiba huo ndipo Kevin alipopata nafasi ya kumwona kwa macho Jackson Motown, akilia kama mtoto mdogo, kifo cha Mario Pizaro kilionekana kumuumiza sana! Akajaribu kadiri ya uwezo wake wote kumfikia lakini haikuwezekana, walinzi walimzuia, alitaka kumuuliza kama alikuwa na fununu za mahali Catarina alipokuwa.
“Nitamfuata huko huko Miami anakoishi!” aliwaza Kevin moyoni mwake.
Hakuna mtu aliyejihusisha naye kwenye mazishi hayo, alibana kwenye kona moyo wake ukiendelea kuumia na mazishi yalipofikia mwisho aliondoka na kurejea mtaani kwake Bronx, akalala mtaani hapo kama kawaida yake na baadaye kupiga simu nyumbani Tanzania akiwapa taarifa ya yaliyokuwa yakiendelea.
“Uwe makini mwanangu, nahisi kuna mtu anayefanya mauaji hayo, kama kweli alichokueleza jirani kuwa Mario Pizaro hakuwa mtumiaji wa pombe wala dawa za kulevya, wakigundua uko hapo wanaweza kukudhuru!” mama yake Kevin alimwambia.
“Niombeeni sana mama.”
“Lakini kwa nini usikubaliane na kilichotokea urudi nyumbani uendelee na masomo yako?”
“Sawa mama, lakini siwezi kufanya hivyo, haya maumivu niliyonayo ni kama Mkuki Moyoni Mwangu!”
“Basi kila la kheri, tunaendelea kukuombea, Mungu atakulinda!”
“Ahsante mama.”
Mchana wa siku iliyofuata alikuwa ndani ya ndege la Shirika la Ndege la United Airlines akieleka Miami, kichwani mwake kama kawaida alikuwa akimfikiria Catarina, moyo wake ulimwambia alikuwa hai mahali fulani, akipata mateso na alihitaji msaada wake. Kama angefanikiwa kukutana na Jackson Motown na kufanya naye mahojiano, pengine angepata taswira ya mahali Catarina wake alipokuwa.
Kando yake aliketi msichana mrembo wa Kizungu, mrefu mwembamba ambaye kila walipoangaliana, macho yao yaligongana, mwisho Kevin akatabasamu na msichana huyo akafanya vivyo hivyo, huo ndiyo ukawa mwanzo wa mazungumzo kati yao.
“Call me Kevin!” (niite Kevin!)
“Call me Mariana!” (Niite Mariana!) alijibu msichana yule uso wake ukiwa umejawa na tabasamu.
“Do you live in Miami?” (Unaishi Miami?)
“Yes, what about you?” (Ndiyo, vipi kuhusu wewe?)
“Can’t you learn something from my accent?” (Huwezi kujifunza kitu fulani kutoka kwenye lafudhi yangu?)
“No! You sound American!” (Hapana! Unaongea kama Mmarekani!)
“No way, I am an African from Tanzania!” (Hapana! Mimi ni Mwafrika kutoka Tanzania)
“Mambo?”
“Do you know that?” (Unaijua hiyo?)
“Yeah! I was in Tanzania last month, I know Ugale, walii and kukyu!” (Ndiyo! Nilikuwa Tanzania mwezi uliopita, najua ugali, wali na kuku!)
“Wow! I can’t believe I am speaking to someone who knows my country!” (Wow! Siwezi kuamini naongea na mtu anayefahamu taifa langu!)
“I know Tanzania, beautiful country, peaceful, Jakaya Kikwete is president! What are you going to do in Miami?” (Naijua Tanzania, nchi nzuri, yenye amani, Jakaya Kikwete ndiye rais wake! Unakwenda kufanya nini Miami?) msichana huyo alimuuliza Kevin.
“Do you know a person by the name of Jackson Motown?” (Unamfahamu mtu anayeitwa Jackson Motown?)
“Yeah! A rich guy but I have never met him! Are you visiting him?” (Ndiyo! Kijana tajiri, ingawa sijawahi kumwona! Unamtembelea yeye?)
“It is a long story!” (Ni habari ndefu!)
“Have you been to Miami before?” (Umeshawahi kufika Miami kabla?)
“No!” (Hapana!)
“You can stay in my house, I have a big apartment, don’t worry about accommodation, I can host you!” (Unaweza kukaa nyumbani kwangu, nina nyumba kubwa, usiwe na mashaka juu ya mahali pa kuishi, nitakuwa mwenyeji wako!)
“What a privilege!”(Bahati kubwa sana!)
Kevin alikubali kufikia nyumbani kwa Mariana akiamini msichana huyo ndiye angesaidia sana kufikia nyumbani ama ofisini kwa Jackson Motown kwa sababu alikuwa mwenyeji, isitoshe kufanya hivyo kungempunguzia gharama ya kuishi kwenye mji wa kitalii wa Miami, ndege ilipotua walishuka pamoja na kutoka nje ambako walichukua teksi iliyowapeleka moja kwa moja hadi nyumbani kwa Mariana.
Kilichowashangaza ni gari jingine lililokuwa likiwafuatilia kwa nyuma mpaka walipofika nyumbani kwa Mariana ndipo nalo likageuza na kuondoka, hawakuweza kuwaona watu waliokuwa ndani ya gari hilo sababu lilikuwa na vioo vilivyozuia mtu wa nje kuona ndani.
***
“Hellow Jackson!”
“Yes!” (ndiyo!)
“He is coming to Miami by United Airlines flight 424, arriving there at 6 PM, make sure the boys at the airport before, I have sent his photo to Dragon!” (Anakuja Miami kwa ndege ya United Airlines namba 424, atafika hapo saa kumi na mbili ya jioni, hakikisha vijana wako uwanja wa ndege kabla, nimetuma picha yake kwa Dragon!)
“Thank you! He will be dead like the others before next morning, I am determined to keep this secret!” (Ahsante! Atakuwa amekufa kama wenzake kabla ya asubuhi kufika, nimedhamiria kuificha siri hii!) ilikuwa ni sauti ya Jackson Motown akifura kwa hasira.

Je, nini kitaendelea? Kevin atakuwa salama? Gari lililowafuatilia ni la nani? Fuatilia kesho katika Gazeti la Championi Jumamosi.

Leave A Reply