The House of Favourite Newspapers

Mradi uliotumbua 6 NSSF ni huu!

0

NSSF (8) Na Hashim Aziz, UWAZI

DAR ES SALAAM: Wakati nafasi za wakurugenzi sita, mameneja watano na mhandisi mmoja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) zilizoachwa wazi baada ya wahusika kusimamishwa zikiwa tayari zimejazwa, Uwazi limeuchimba kwa kina mradi uliowaponza vigogo hao waliosimamishwa hivi karibuni.

Chiku Chiku Matesa

Mwishoni mwa wiki iliyopita, mwandishi wetu alifunga safari mpaka Dege, uliko mradi wa Ujenzi wa Mji Mpya wa Kigamboni (Dege Eco Village) – (pichani) ambao unatajwa kuwa ndiyo uliosababisha kutumbuliwa kwa vigogo hao na kuzungumza na wakandarasi na wafanyakazi waliokuwa wakishiriki kwenye mradi huo.

KidullaYacoub Kidula

WALIANZA HIVI

“Huu mradi kwa kweli ulikuwa na figisufigisu nyingi sana. Mimi binafsi nilikuwa nafanya kazi kama kibarua na kuna mambo mengi tu nilikuwa naona hayaendi sawa,” kilisema chanzo kimoja kilichoomba hifadhi ya jina lake.

Crescentius MagoriCrescentius Magori

Chanzo hicho kiliendelea kutiririka kwamba, kabla ya kuanza kwa mradi huo, eneo halikuwa na shughuli yoyote ya msingi lakini mradi ulipoanza, vigogo wengi serikalini, walianza kununua viwanja vikubwa kwenye maeneo ya kuzunguka mradi na kuporomosha majumba ya kifahari.

“Si unaona majumba ya watu binafsi yalivyoporomoshwa kwa wingi upande wa pili wa mradi? Hawa wote hakuna mkazi wa Dege hata mmoja, ni watu wa serikalini. Mradi wenyewe una magorofa kama 40 hivi,” kiliendelea kutiririka chanzo chetu.

MrossooLudovick Mrosso

MAFUNDI WALIUTABIRIA

Fundi mwingine aliyejitambulisha kwa jina moja la James, yeye alisema walishajua kwamba mradi huo hauwezi kukamilika kutokana na mambo mbalimbali yaliyoashiria hivyo (hakuyasema).

 “Unajua kabla mradi haujasimamishwa, tulikuwa tunafanya kazi sehemu mbilimbili, yaani kwenye mradi na kwenye nyumba za baadhi ya vigogo wa serikalini. Kwa hiyo tulihisi kuna mambo hayaendi sawasawa sana.

NSSF (2) “Mi naona hata serikali yenyewe ilichelewa kushtuka mapema. Lakini kwa vile wamesimamishwa, uchunguzi ufanyike kuona nani alikosa, naamini wapo waliosimamishwa hawahusiki lakini kuna wanaohusika, wapo kazini,” alisema fundi huyo.

NSSF (1)UWAZI LAWATAFUTA WAHUSIKA

Baada ya kusikia maelezo hayo, Uwazi lilifanya jitihada za kuwapata vigogo waliotumbuliwa. Hata hivyo, kazi ya kuwapata vigogo hao ana kwa ana haikuwa nyepesi.

Uwazi lilifanikiwa kupanga ‘appointment’ ya kukutana na Yacob Kidula, aliyekuwa Mkurugenzi wa Mipango, Uwekezaji na Miradi ambapo licha ya makubaliano ya kukutana, simu ya kigogo huyo haikuwa ikipatikana hewani na hata ilipopatikana, haikuwa ikipokelewa.

NSSF (4)Mwandishi wetu alifanya jitihada za kumtumia ujumbe wa maandishi kigogo huyo akimsisitiza kuhusu kukutana naye au kuzungumza chochote kuhusu kusimamishwa kwake lakini hakujibu mpaka gazeti hili linakwenda mitamboni.

KUTOTAKA KUZUNGUMZA

Kuna taarifa kuwa, vigogo hao hawako tayari kuzungumza lolote kwa vile, suala lao linachunguzwa na vyombo husika ili kubaini ukweli wa madai yao na endapo wataonekana hawana hatia, watarudishwa kazini.

NSSF (3)TUJIKUMBUSHE

Hivi karibuni, bodi ya wadhamini ya NSSF inayoongozwa na Profesa Samuel Wangwe, iliagiza kusimamishwa kazi kwa wakurugenzi sita, mameneja watano na mhandisi mmoja wa shirika hilo ili kupisha uchunguzi baada ya kubainika kuwepo kwa vitendo vya ubadhirifu, matumizi mabaya ya ofisi na kutofuata kanuni, sheria na taratibu katika uwekezaji, usimamizi wa miradi, manunuzi ya ardhi na ajira.

NSSF (6)Wakurugenzi sita waliosimamishwa kazi na nafasi zao kwenye mabano ni Kidula (Mkurugenzi wa Mipango, Uwekezaji na Miradi), Ludovick Mrosso (Mkurugenzi wa Fedha), Chiku Matessa (Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala) na Sadi Shemilwa (Mkurugenzi wa Udhibiti Hadhara na Majanga).

Wengine ni Pauline Mtunda (Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Mahesabu ya Ndani) na Crescentius Magori (Mkurugenzi wa Uendeshaji) sambambana mameneja wengine watano na mhandisi mmoja.

NSSF (7)Kabla ya kutumbuliwa vigogo hao, mradi huo ulisimamishwa na serikali Aprili, mwaka huu baada ya kubainika kuwepo kwa upotevu wa zaidi ya shilingi bilioni 179.

Mradi huo ulikuwa ukisimamiwa na Kampuni ya Hifadhi Builders LTD iliyokuwa chini ya NSSF kwa ushirikiano wa Azimio Housing Estate Limited, mkandarasi akiwa ni M/s Mutluhan Construction Industry Company Limited kutoka Uturuki.

Leave A Reply