The House of Favourite Newspapers

Salman Khan wa Bollywood aachiliwa huru

0

Indian Bollywood actor Salman Khan (2R) celebrates and wishes his fans Ramzan Eid Mubarak at his residence in Mumbai on July 18, 2015.  AFP PHOTO        (Photo credit should read STR/AFP/Getty Images)

Bombay, India

Mmoja wa nyota wa kuigiza filamu nchini India, Salman Khan, ameachiliwa na mahakama moja kwa kosa la kumpiga risasi na kumuua mnyama wa mwituni aliye katika hatari ya kuangamia kabisa duniani.

Alikuwa ameshtakiwa kwa kuwaua swara watatu katika jimbo la Kaskazini la Rajasthan mwaka wa 1998. Mwaka uliopita aliachiliwa na mahakama kwa kosa jingine la kumkanyaga na kumuua mtu asiye na makaazi.

Salman Khan, ni nyota wa filamu kutoka kundi la waigizaji la India, maarufu Bollywood, ambaye ana sifa ya kujikuta mashakani mara kwa mara. Mwaka 1998 alilaumiwa na kabila moja la Rajasthan kwa kupiga risasi na kuwaua swara watatu wakati alipokuwa katika shughuli za uwindaji.

Swara hao wanalindwa kisheria na pia wanasujudiwa na kabila lililoshtaki. Alikuwa amepatikana na kosa na mahakama ya chini na kuhukumiwa kifungo lakini sasa ameachiliwa baada ya kukata rufaa.

Mwaka uliopita, nyota huyo anayejipata mashakani mara kwa mara aliachiliwa na mahakama kwa kosa la kumkanyaga kwa gari mtu asiye na makaazi alipokuwa akiendesha gari lake.

Leave A Reply