The House of Favourite Newspapers

Msanii yamkuta mazito

0

Na Dustan Shekidele,
Risasi Jumamosi

Morogoro: Msanii maarufu wa muziki wa dansi mkoani hapa, Josse Kigenda yamemkuta mazito baada ya kuvamiwa nyumbani kwa hawara yake aliyetajwa kwa jina moja la Grace.
Tukio hilo la aina yake lilijiri hivi karibuni majira ya saa 6:00 mchana, nyumbani kwa Grace na mumewe Mwandaba, maeneo ya Modeko mjini hapa ambapo mwanamuziki huyo alikutwa mtupu kitandani kwa wanandoa hao.
Kwa mujibu wa mashuhuda, Mwandaba aliyeeleza kuwa alifunga ndoa ya bomani na Grace, akiwa na timu yake, alifika nyumbani hapo kisha kumvaa jamaa huyo na kumfanyia kitu mbaya kwa kumshushia kipigo ‘hevi’ huku wakimpiga picha za utupu.
Akizungumza na mwanahabari wetu juu ya tukio hilo, mume wa Grace alitiririka: “Mimi ni mfanyabiashara, nazunguka mikoa mbalimbali nchini, naweza kutoweka nyumbani zaidi ya miezi mitatu hadi minne.
“Siku za hivi karibuni, nikiwa safarini, nilipokea taarifa kutoka kwa marafiki zangu kuwa mwanamuziki Kigenda anatembea na mke wangu, mbaya zaidi amemfundisha kuimba ambapo hupanda jukwaani na kuniimba nyimbo za mafumbo kwamba mwanaume mashine siyo sura.
“Baada ya kupokea taarifa hizo za kuumiza, ghafla nilirudi nyumbani bila kumtaarifu mke wangu.
“Huwezi kuamini, nilipoingia chumbani nilimkuta Kigenda amelala kitandani uchi wa mnyama, ukweli nilimpa vitasa vya maana.”
Baada ya kumsikia mume wa Grace, gazeti hili lilimtafuta msanii Kigenda ili kuzungumzia mkasa huo ambapo mbali na kukiri kukutwa na figisufigisu hiyo alikuwa na haya ya kusema: “Wewe Shekidele (jina la mwandishi wetu) siyo mgeni kwangu, siku zote unaniona kwenye kumbi za starehe na Grace na umekuwa ukinipiga picha jukwaani nikiimba naye na muda wote natumia gari lake.
“Kweli (Grace) aliwahi kunitamkia kuwa ameolewa na Mwandaba lakini alidai walishaachana baada ya huyo jamaa kumtapeli shilingi milioni 80, akawa ananiambia nimuoe, nilimkatalia kwa kuwa nina mke.
“Siku ya tukio nililala kwake (Grace), nashangaa saa sita mchana nikavamiwa na jamaa aliyedai kuwa ni mume wa Grace na kuanza kunipiga akidai eti amenifumania. Nashukuru watu walioniokoa na kunisitiri nikarudi kwangu lakini nilikuwa nyang’anyang’a kwa kipigo.”
Kwa upande wake Grace ambaye tukio hilo lilifanyika nyumbani kwake anayedaiwa kuwa na fedha ndefu alikuwa na haya ya kusema: “Ni kweli tukio hilo limetokea nyumbani kwangu lakini ninachokiona ni kwamba wanaume wote wawili wamekuja kufanyiana fujo kwangu.
“Huyo anayedai ni mume wangu ni kweli nilifunga naye ndoa ya bomani ambayo ilidumu kwa miezi mitatu tu kwani baada ya kugundua nina fedha aliomba nimkopeshe shilingi milioni 80. Kwa kuwa ni mume wangu nilimpa lakini alinikimbia, nilimtafuta kwa zaidi ya miezi mitatu bila mafanikio.
“Niliamua kumsamehe lakini nashangaa anakuja kwangu ghafla na kumfanyia fujo Kigenda, bila kumuamulia angemuua kaka wa watu.
“Kigenda ni mpenzi wangu hata kabla sijaolewa na huyo jamaa, tatizo Kigenda hakuwa tayari kunioa hivyo tulikubalina nikipata mwanaume wa kuniona nifanye hivyo na kweli baada ya kumpata huyo jamaa nilimwambia Kigenda, tukaachana kwa amani.
“Sasa huyo jamaa aliponikimbia na fedha zangu nikaamua kurudi kwa Kigenda.”
Hata hivyo, hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, Grace aliahidi kwenda kuripoti tukio hilo polisi.

Leave A Reply