The House of Favourite Newspapers

Stoo ya mfanyabiashara yateketea kwa moto usiku

0

1.Moto ulivyoonekana ndani ya stoo hiyo iliyoungua.-001 Moto ulivyoonekana ndani ya stoo hiyo iliyoungua.

2.Geti la kuingilia ndani ya stoo hiyo lilivyoonekana.-001Geti la kuingilia katika stoo hiyo lilivyoonekana.

3.Kikosi cha zima moto kilivyoonekana kupambana na m oto huo.-001Kikosi cha Zimamoto kilivyoonekana kupambana na moto huo.4.-001

5.Gari la zima moto likiwa eneo hilo la tukio.-001Gari la Zimamoto likiwa eneo hilo la tukio.

6Baadhi ya watu walishuhudia tukio hilo la kuungua stoo hiyo.-001Baadhi ya watu walioshuhudia tukio hilo.

7.Moto ukiteketeza jengo hilo.-001Moto ukiteketeza jengo hilo.

8.Kikosi kazi cha zima moto kikihakikisha kinaudhibiti moto huo.-001Kikosi kazi cha zima moto kikihakikisha kinaudhibiti moto huo.

9.-001Askari wa Zimamoto wakihakikisha wanaudhibiti moto huo.

10.Hali halisi ya tukio hilo.-001Hali halisi ya tukio hilo.

11.-001

12.-001

13.-001

14.Gari la zima moto likiwa eneo la tukio.-001Gari la Zimamoto likiwa eneo la tukio.

STOO ya mfanyabiashara mmoja jijini Dar es Salaam aliyefahamika kwa jina moja la Mushi iliyokuwa katika Barabara ya Kijitonyama karibu na Kituo cha Polisi cha Kijitonyama ‘Polisi Mabatini’ imeteketea kwa moto mishale ya saa nane usiku.

Kwa mujibu wa majirani walio karibu na stoo hiyo walisikika wakisema ndani yake kulikuwa na vitu mbalimbali vya dukani na ilikuwa bado mpya.

Akizungumza na mwandishi wetu mlinzi wa Kimasai wa stoo hiyo ambaye hakujitambulisha jina, alisema chanzo cha moto huo anahisi ni hitilafu ya umeme iliyotokana na cheche za umeme ndani ya stoo hiyo.

Akifafanua zaidi mlinzi huyo alisema kabla ya moto huo kulipuka kulikuwa na mafundi wa umeme waliokuwa wakiunga nyaya ambao waliondoka na baada ya muda mfupi cheche zilionekana kwenye nyaya za umeme katika stoo hiyo.

Baadaye Kikosi cha Zimamoto kilifika na magari matatu kuzima moto huo.

NA DENIS MTIMA/GPL

Leave A Reply