The House of Favourite Newspapers

Mshindi wa Nyumba Nelly Mwangosi Kukabidhiwa Mjengo J5

0

Nyumba-10Mjengo atakaokabidhiwa Nelly Mwangosi, uliopo Salasala nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Stori: Mwandishi Wetu, Wikienda

YULE mshindi wa droo kubwa ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba, iliyoendeshwa na Global Publishers Ltd kwa muda wa miezi sita, hatimaye atakabidhiwa mjengo wake wenye thamani ya mamilioni, uliopo Salasala nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

nellys2Nelly Mwangosi kushoto akiwa na familia yake

Nelly Mwangosi, mama wa watoto wawili mwenyeji wa mkoani Iringa, aliibuka kidedea katika droo ya mwisho iliyochezeshwa Mbagala Zakhem, jijini Dar es Salaam Juni 30, mwaka huu na kuhudhuriwa na mamia ya wasomaji wa magazeti ya Global Publishers ambayo ni Championi, Ijumaa, Risasi, Amani, Uwazi na Ijumaa Wikienda.

nellys…Akiwa na mumewe

Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho alisema jana kuwa mambo mengine yote muhimu kuhusu makabidhiano hayo ya nyumba yamekamilika na kwamba mshindi huyo atapewa nyumba yake hiyo Jumatano ya Julai 27, mwaka huu.

“Tuliahidi na lazima tutekeleze, kama tulivyosema hapo nyuma, tumedhamiria kwa dhati kabisa kurejesha kidogo tunachokipata kwa wasomaji wetu ambao wametoa mchango mkubwa kwa kampuni yetu kwa kipindi chote cha uwepo wake.

Nyumba-2Mtakumbuka hii siyo mara ya kwanza kwa sisi kuandaa bahati nasibu kama hii, tumeshafanya hivyo mara nyingi na leo haiwezi kuwa mara ya mwisho.

Nyumba-9“Tutaendelea na mpango huu, mwisho wa bahati nasibu hii ni mwanzo wa bahati nasibu nyingine, ninachoweza kusema ni kuwaambia wasomaji wetu kuwa wakati wowote tutawaletea kitu kingine ambacho kitakuwa ni chenye manufaa kwao, tunaomba waendelee kutuunga mkono,” alisema meneja huyo.

Droo ya shinda nyumba ilianza Desemba mwaka jana kwa kuhusisha droo ndogo nne ambazo wasomaji walijishindia zawadi ndogondogo nyingi zikiwemo pikipiki, vyombo vya jikoni, mashuka, tv flat screen na vingine vingi.

Nyumba-3Irina mwenye umri wa miaka 45, ambaye amekuwa msomaji wa magazeti pendwa ya Global Publishers kwa zaidi ya miaka 18, wakati akifahamishwa kuhusu ushindi wake, alisema hiyo ilikuwa ni bahati nasibu yake ya kwanza kushiriki licha ya kampuni kuwa nazo nyingi, zilizohusisha magari ya aina mbalimbali, pikipiki, televisheni na kadhalika.

Nyumba-4“Nilipopigiwa simu ya ushindi, sikumuambia mtu yeyote kwa kuwa sikuamini, nilimwambia mume wangu pekee na kukubaliana kusubiri kuona nini kingeendelea, nilipoona jina langu limeandikwa gazetini kuwa ni mshindi, ndipo nikaanza kuwaambia ndugu zangu, nimefurahi sana kwa kweli,” alisema mshindi huyo ambaye hakuwahi kuwa na ndoto za kumiliki nyumba jijini Dar es Salaam.

Nyumba-8Nyumba atakayokabidhiwa mshindi huyo, yenye vyumba vitatu, sebule, jiko, bafu na choo, ina samani za kisasa ndani yake, kitu ambacho kitamfanya kuweza kuingia na kuanza maisha pasipo na haja ya kununua fenicha mpya.

Leave A Reply