The House of Favourite Newspapers

Omog, Pluijm, Mzungu wa Azam nani kuondoka mapema?

0

Joseph-Marius-OmogKocha wa Simba, Joseph Omog enzi akiwa Azam FC.

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam – Championi Jumamosi

KUNA ugumu fulani hapa, lakini lazima mmoja wao atafungashiwa virago endapo timu yake haitakuwa na uvumilivu kutokana na matokeo mabaya, pia nafasi itakayokuwanayo katika msimu ujao wa Ligi Kuu Bara baada ya mechi kumi za kwanza.

pluijmPluijm wa Yanga ambaye ni raia wa Uholanzi.

Ni kama wanaanza sawa, kwani Kocha wa Simba, Joseph Omog, wa Yanga, Hans van Der Pluijm na yule wa Azam FC, Zeben Hernandez wote wamesaini mkataba wa miaka miwili kuzitumikia timu zao. Omog ni raia wa Cameroon, hivyo analijua soka la Afrika vizuri kama ilivyo kwa Pluijm wa Yanga ambaye ni raia wa Uholanzi lakini amekaa sana Ghana na kuzijua tabia kibao za wachezaji wa Kiafrika.

 

Hernandez yeye ni raia wa Hispania na wengi wanasubiri kuona Azam ikicheza soka la Kihispania uwanjani bila kujali aina ya wachezaji ilionao kikosini.

AZAM (5)

Kocha wa Azam FC, Zeben Hernandez akiwa na wachezaji wake.

Kwa miaka minne sasa, Simba haijatwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara na sasa Omog anatarajiwa kuleta mapinduzi wakati Yanga inategemea kuendelea kung’ara chini ya Pluijm aliyeipa ubingwa msimu uliopita. Yanga ipo katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika lakini haina mwenendo mzuri katika Kundi A ikiwa na pointi moja tu halafu ipo mkiani.

 

Timu zote tatu zina historia ya kutovumilia kukaa na kocha kwa muda mrefu endapo mwenendo wa timu utaonekana si wa kuridhisha iwe kwa sare nyingi au kupoteza michezo.
Katika ratiba mpya ya ligi kuu itakayoanza Agosti 20, mwaka huu, Yanga imepangwa kuanza na JKT Ruvu kisha itacheza na African Lyon halafu Ndanda FC. Pia Yanga itacheza na Majimaji FC halafu Mwadui. Mechi za Simba ni dhidi ya Ndanda, JKT Ruvu, Ruvu Shooting, Mtibwa Sugar kisha na Azam. Azam yenyewe inaanza na African Lyon, Majimaji, Prisons, Mbeya City na Simba. Baada ya hizo mechi tutapata jibu

Leave A Reply