The House of Favourite Newspapers

Taasisi za Serikali, Dini na Kiraia Zatakiwa Kufuata Maadili

maadili-1-1Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Suzan Mlawi, akizungumza jambo kwenye hafla hiyo.

maadili-2-1Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Ayoub Rioba (kushoto) akichangia mada katika hafla hiyo.

maadili-3-1Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba, akihojiwa na wanahabari kuhusiana na mdahalo huo.

maadili-4-1Suzan Mlawi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mdahalo huo.

Na Denis Mtima/GPL

NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Suzan Mlawi,  amezitaka taasisi za serikali, dini na asasi za kiraia kufuata maadili yanayotakiwa katika kazi zao.

Hayo ameyasema leo wakati  akizindua mdahalo wa asasi hizo uliofanyika kwenye Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam uliojadili mada mbalimbali hasa zilizokuwa zikilenga masuala ya maadili na haki za binadamu kuelekea maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu yanayotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Comments are closed.