TanEA Yaanika Tathmini Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Ofisa wa TanEA, Wallace Mayunga akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).

 

TAASISI binafsi ya TanEA ambayo ni muunganiko wa Asasi mbili za kiraia, Action for Change (ACHA) na The Right Way (TRW) zilizoungana ili kutoa elimu ya uraia, elimu ya mpiga kura, na uangalizi wa uchaguzi  baada ya kupata kibali kutoka Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imeufanyia utafiti uchaguzi wa serikali za mitaa uliopita na kutoa mapendekezo kadhaa.

 

 

Taasisi hiyo kwa kutumia maofisa wake 150 kufanya tathmini kwenye mikoa 13 ya Tanzania Bara na wilaya zipatazo 40.

 

Baadhi ya mambo yaliyobainika ni kama yafuatayo;

  • Kufanyika kwa kampeni huru zenye utulivu ambapo wagombea na vyama vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi havikutawaliwa na vitisho wala rushwa.
  • Wagombea kufuata taratibu na mwenendo unaowaongoza kufuata kanuni na maadili ya mchakato wa uchaguzi.
  • Vyama na wagombea kupatiwa haki sawa ya kusikilizwa.
  • Vyama na wagombea wanaoshindana kupatiwa fursa sawa za kusambaza ujumbe wao kupitia njia mbalimbali.
  • Pamoja na hayo Mayunga amesema dosari zilizojitokeza ni pamoja na watendaji kutokuwepo kwenye vituo vya kujiandisha muda wa kazi, wagombea wengine kujitoa kwenye uchaguzi na nyinginezo.

HABARI: NEEMA ADRIAN

PICHA: RICHARD BUKOS/GPL


Loading...

Toa comment