The House of Favourite Newspapers

TCRA Yawataka Kwenda Shule Kabla ya 2022 – Video

0

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya  mawasiliano Tanzania TCRA,  Mhandisi James Kilaba amewataka waandishi wa habari kote nchini kuhakikisha wanajiendeleza kielimu kabla ya Desemba 30, mwaka 2021 ambapo sheria inayosimamia taaluma ya Habari na Utangazaji itaanza kufanya kazi.

 

Kilaba ameyasema hayo leo Desemba 4, 2019 katika kongamano na wanachama wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Mwanza (MPC) katika kongamano lililofanyika kwenye ukumbi wa Nyanza jijini Mwanza.

Akizungumza katika kongamano hilo lililokuwa na lengo la kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuelewa sheria zinazosimamiwa na TCRA, Mhandisi Kibala amesema ili mwandishi aweze kutambulika lazima awe amesoma angalau kuanzia ngazi ya dipoloma ya uandishi wa habari.

 

“Nawaomba waandishi wote hapa nchini kupitia mkutano huu kwamba kwa mujibu wa kifungu cha 19 (1) cha sheria ya vyombo vya habari mwaka 2016 kufanya kazi kama mwaandishi wa habari  wa habari pasipo kuthibitishwa kwa mujibu wa sheria  ni kuvunja sheria.

 

“Kwa mujibu wa kanuni ya 17 (2) ya kanuni za vyombo vya habari mwaka 2017 ili mtu athibitishwe kuwa mwandhishi  pamoja na mambo mengine anatakiwa kuwa na Shahada au Astashahada ya uandishi wa habari au inayohusiana na maswala ya Vyombo vya habari  kutoka katika chuo kinachotoa elimu ya maswaa hayo ,” alisema Kilaba.

 

“Kwa upande wake Mkurugenzi wa klabu za Uandishi wa habari hapa nchini UTPC Abubakar Karsan amesema kwa sasa sheria inatumika hivyo waandishi wa habari lazima wakubali ukweli.

“Kwa sasa sheria ya vyombo vya habari inafanya kazi hivyo ni wajibu kwa waandishi wa habari kujiendeleza kabla ya muda ambao tumepewa ambapo ni Desemba 30, mwaka 2021 tangu Desemba 31, mwaka 2016 lilipotolewa tamko lakini sisi kama wasimamizi wa klabu za waandishi wa habari hapa nchini tunaendelea na jitihada za kuhakikisha hata hawa wenye certificates nao kutambulika japokuwa kazi bado ni kubwa mno.”

 

 

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza (MPC), Edwin Soko amesema chama chake kimejipanga kuhakikisha kinatengeneza mazingira ya wanachama wake kuendelezwa.

“Sisi kama MPC tutapambana kuhakikisha tunatafuta namna ambayo tutawaendeleza wanachama wetu kwani tutafanya utaratibu ambao utakuwa wezeshi kwa kila mmoja kujiendeleza kupata elimu ya Diploma ambayo inatakiwa na sheria ya vyombo vya habari.”

 

Na Johnson James- GPL MWANZA.

Leave A Reply