The House of Favourite Newspapers

Uni Bash Carnival ya +255 Global Radio Yatikisa UDSM – Pichaz

0
Mtangazji wa kipindi cha Bongo 255 cha +255 Global Radio, Stewart George (kushoto) akimkabidhi zawadi ya kitabu cha Eric Shigongo, mwanafunzi wa UDSM baada ya kupakua app ya +255 Global Radio kwenye simu yake.

NOVEMBA 29, 2019, ilikuwa siku ya kihistoria na kiburudani kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), baada ya radio ya mtandaoni inayotamba kwa sasa nchini, +255 Global Radio kufika chuoni hapo kuzungumza na wanafunzi hao na kufanya bonge la tamasha lililopewa jina la Uni Bash Carnival.

Watangazji wa +255 Global Radio, Gabby Mtanzania (kushoto) na Stewart George (kulia) wakiwa na mwanafunzi wa UDSM (katikati) wakimkabidhi zawadi ya kitabu cha mtunzi mahiri, Eric Shigongo,  baada ya kupakua App ya +255 Global Radio.

Timu nzima ya +255 Global Radio ambao ndiyo waandaji wa tamasha hilo ilijumuika na wanafunzi wa chuo hicho ili  kuwaburudisha na kuwaelimisha kuhusu mabadiliko makubwa ya teknolojia ya habari na mawasiliano.

Watangazaji kutoka +255 Global Radio wakiserubuka wakati wa ufunguzi wa Tamasha la Uni Bash Carnival lililofanyika viwanja vya UDSM.

Katika tamasha hilo lililofanyika kwenye viwanja vya chuo hicho huku kukiwa na burudani za kutosha kutoka kwa Ma-DJ wakali, zawadi kemkem, wanafunzi hao pia walipewa elimu kuhusu namna ya upatikanaji wa matangazo ya moja kwa moja ya +255 Global Radio ambayo inatumia mfumo wa teknolojia ya mtandaoni kurusha matangazo yake.

 

Mtangazaji wa kipindi cha Bongo 255 cha +255 Global Radio, Lady Mufasa (kulia) akimkabidhi zawadi ya kitabu mwanafunzi wa UDSM baada ya kujibu swali kwa ufasaha.

Sambamba na hayo  +255 Global Radio ilifanikiwa kunadi vipindi vyake vyote vinavyoruka redioni kwa wakati tofauti tofauti ndani ya saa 24 siku saba za wiki.

Wanafunzi wa USDM wakiwa na zawadi zao za vitabu.

Aidha katika tamasha hilo wanafunzi wa UDSM waliweza kufundishwa namna ya kusikiliza na kupakua Aplikesheni ya redio kupitia simu zao za mkononi na kompyuta.

Baadhi ya wanafunzi  wakiwa kwenye tamasha la Uni Bash Carnival.

Baadaye burudani kali ilishushwa na ma-DJ mahiri kutoka +255 Global Radio wakiongozwa na DJ Super, DJ Big Daddy na DJ Obway, sambamba na utambulisho wa watangazji wote wa vipindi kutoka +255 Global Radio chini ya meneja wao, Borry Mbaraka.

 

…Wakimsikiliza mtangazaji kutoka +255 Global Radio, Gabby Mtanzania.

Tamasha hilo lililodumu kwa saa sita lilifana na kujenga mahusiano mema na uongozi wa UDSM na wanafunzi kwa jumla.

 

Mmoja wa wanafunzi wa UDSM akipakua App ya +255 Global Radio kwenye simu yake.

24/7 #Tunakusanua Kinachoendelea Kwenye Ulimwengu Wa Burudani | Kutusikiliza au kupakua app ya radio Bonyeza Hapa bit.ly/_255GlobalRadio

Wanafunzi wakimiminika kushiriki tamasha la Uni Bash Carnival.

 

Meneja wa +255 Global Radio, Borry Mbaraka akitoa maelekezo ya kupakua App ya Radio hiyo kwa wanafunzi hao.

 

Leave A Reply