The House of Favourite Newspapers

Yanga Yaichapa African Lyon 3-0

0

Yanga vs African Lyon (4)

Beki wa Yanga, Hassan Kessy akimiliki mpira mbele ya wachezaji wa Yanga SC.

Yanga vs African Lyon (5)

Wachezaji wa Yanga wakishangilia mojawapo ya mabao yao.

Yanga vs African Lyon (6)

Mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe akijaribu kuitoka ngome ya African Lyon.

Yanga vs African Lyon (7)

Simon Msuva akikwaana na beki ya African Lyon.

Yanga vs African Lyon (2)

Kikosi cha Yanga kilichoanza kukwaana na African Lyon leo.

Yanga vs African Lyon (1)

Kikosi cha African Lyon kilichoanza dhidi ya Yanga leo. 

Yanga vs African Lyon (3)

Benchi la African Lyon.

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga SC leo wameanza vizuri ligi hiyo baada ya kuishushia kichapo cha mabao 3-0 timu ya African Lyon katika mechi iliyopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Alikuwa Deus Kaseke aliyeanza kuipatia Yanga bao la kwanza baada ya mabeki wa Lyon kujua ameotea katika dakika ya 18 ya mchezo huku Simon Msuva akifunga bao la pili dakika ya 60 akipokea pasi ndefu kutoka kwa Thaban Kamausoko.

Juma Mahadhi alipigilia msumari wa mwisho kwa African Lyon baada ya kuipatia Yanga bao la tatu akipokea pasi safi kutoka kwa Yusuph Mhilu katika dakika ya 90.

Hadi mwisho wa mchezo, Yanga 3, African Lyon 0.

Picha zote na Richard Bukos / GPL

Leave A Reply