The House of Favourite Newspapers

Yanga yamwita Coutinho Dar

0

coutinho-shangwe-za-goalMbrazili, Andrey Coutinho.

Nicodemus Jonas, Dar es Salaam
UKISIKIA nyani mzee kukwepa mishale mingi maishani ndiko huku kwa filamu inayoendelea kwa Mbrazili, Andrey Coutinho na Yanga. Awali kulikuwa na taarifa kuwa nyota huyo ataonyeshwa mlango wa kutokea, lakini mambo yamegeuka ghafla na jamaa muda wowote anatua Bongo.

Winga huyo anayehimili kucheza wingi ya kushoto amepitia majaribu mengi tangu kuanza kwa msimu huu, ambapo almanusra kutemwa lakini akabaki kwa kile kilichotajwa kuwa ni mkono wa Mwenyekiti, Yusuf Manji.

Hali hiyo ikajirudia kwenye dirisha hili la usajili ambapo amehusishwa kutemwa, lakini Katibu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha ameruka kimanga na kufafanua kuwa tayari Coutinho ameishatumiwa tiketi ya ndege kutua Bongo akitokea kwao Brazil.

“Coutinho bado ni mchezaji wetu jamani na hakuna mpango wa kumuacha. Amechelewa kurejea lakini mipango yote ya safari yake kurejea kikosini imeshafanyika na suala la tiketi limeshakamilishwa, hivyo muda wowote atatua.

“Kama ilikuwa ni kumuacha, basi ilikuwa iwe mwanzoni mwa msimu lakini kwa sasa tuna mipango naye na tutakuwa naye msimu mzima,” alisema Dk Tiboroha.

Leave A Reply