The House of Favourite Newspapers

Dakika 90 hatari zaidi

0

YANGA (2) Omary Mdose,Dar es Salaam
TIMU za Simba na Yanga, leo Jumatano zitashuka dimbani kusaka pointi tatu kwenye muendelezo wa Ligi Kuu Bara ambayo tamati yake ni Mei 7, mwaka huu.
Yanga itaingia uwanjani kucheza dhidi ya Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya, ikiwa na kumbukumbu mbaya ya kupoteza pointi tatu mbele ya Coastal Union baada ya kuchapwa mabao 2-0, wikiendi iliyopita huku Simba ikiingia kupambana na Mgambo JKT katika Uwanja wa Taifa, Dar.
Ligi hiyo ambayo tayari imeshaingia mzunguko wa pili, hizi zitakuwa ni mechi za pili baada ya kuanza kwa mzunguko huo ambao ni wa lala salama.

SIMBA-YANGA-7.jpgYanga ambayo ndiyo kinara wa ligi hiyo ikiwa na pointi 39 sawa na Azam, itahitaji kushinda mchezo huo kwani inafahamu kuwa kama itapoteza na Simba kushinda basi watakuwa wamelingana pointi kutokana na sasa kuwazidi watani zao hao wa jadi pointi tatu pekee.
Yanga leo itawakosa mabeki wake mahiri, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ambaye bado hajapona majeraha yake ya kifundo cha mguu pamoja na Kelvin Yondani anayetumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyopata kwenye mchezo uliopita walipofungwa na Coastal Union mabao 2-0 huku pia taarifa zikisema kuwa Thaban Kamusoko naye ni mgonjwa.

Leave A Reply