The House of Favourite Newspapers

Prof Jay Afunguka Ishu ya Harmonize, Rayvanny – Video

0

 

MKONGWE wa Muziki nchini, Professor Jay, leo Aprili amepiga stori kwenye kipindi cha Bongo 255 cha 255 Global Radio na kufunguka mambo mbalimbali..

 

 

“Tulianza muziki tukichukulia kama hobby tu, lakini tukaanza kubadilisha mentality yake na kufanya muziki uwe njia ya kujiajili. Kushawishi watu wazima kuupenda muziki na kwamba muziki sio uhuni lakini kuna wahuni wachache wanafanya muziki.

Prof. Jay akilakiwa na wafanyakazi wa Global Group alipowasili katika Ofisi hizo kwa ajili ya mahojiano.

 

 

 

 

“Sisi tulikuwa kama burudoza, kuchonga barabara wengine wapite. Kuubadilisha muziki kuwa biashara, sasa hatuwezi kuruhusu tuliyowachongea barabara wakaturudisha nyuma, lazima tuhakikishe tuna-maintain hiyo heshima.

 

 

“Tuendelee kuurudisha muziki kwenye sehemu yake, tuache kupenda ngoma ambazo hazina maadili. Huwezi kukaa na mzazi wako kusikiliza ngoma ambazo ni za chumbani zenye lugha ngumu ngumu. Rapcha ni rapa wa kisasa mwenye uwezi mkubwa sana, na ana tumia akili.

 

 

“Sipendi sana kuimba maisha yangu, ilitokea tu mara moja baada ya mama yangu kufariki kwa kugongwa na gari, niliingiza tu laini hiyo kama kumbukumbu lakini si wimbo mzima, maana ingekuwa kama najiimbia mwenyewe na ingenitia simanzi wakati natakiwa kuwaimbia watu.

 

 

“Nimefanya kazi na Harmonize, ni kijana nayejituma sana na ninaheshimu sana kipaji chake. Lakini kwa kinachoendelea ningeshauri tushindane kwenye kazi, naona kama imevuka pale inaenda person na hii inaleta uhasama.

 

 

“Haya mambo tukishaanza kushabikia mambo ya timu kuna siku Harmonize na Rayvanny watakutana uso kwa uso halafu mambo yatakuwa mabaya zaidi. Hatuko tayari kuona msanii yeyote anapotea ama kuona vipaji hivi vinapotea. Hakuna mtu akafanya bifu ikamsaidia.

 

“Niwaombe mashabiki na wasanii turudi kwenye mstari, tusapoti kazi zao ili iweze kuendelea lakini tusisapoti uchafu unaofanyika.

 

 

“Mameneja wengi wa wasanii unakuta tu kwa sababu ana pesa anataka awekeze kwa msanii ili apige hela, lakini hana idea ya biashara ya muziki. Kuna mameneja wengine wanajua muziki lakini wanataka msanii akimbie haraka kwenye mafanikio.

 

“Meneja wa Meja Kunta ndiye alikuwa wa kwanza kuposti kiki kuwa msanii wake amekufa, sasa itafakari imekaaje hiyo? Msanii anatakiwa kumheshimu sana meneja lakini wasanii wengi hawawaheshimu. Ukiheshimu meneja huwezi kusikia vitu kama hivi vinavyoendelea.

 

 

“Siwezi kusimama nikasema ninaomba Mtaa uitwe jina langu, ni sawa na kukunja ngumi wakati pambano linakwisha. Kuwapa mtaa wasanii ni jambo jema, si wasanii tu hata wanamichezo na watu wengine ambao wamefanya makubwa kwenye nchi yetu. hii inaonyesha kuthaminiwa.

 

 

“Kwanza mimi ni mshindi wa siku zote, miongoni mwa wabunge waliofanya vizuri bungeni na kuwawakilisha wananchi ni Prof. Jay, si kwamba nilishindwa, lakini katika uchaguzi ule wa 2020 sikutangazwa kuwa mshindi.

 

Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho akisalimiana na Prof. Jay.

“Wananchi wa Mikumi wamenipa jina la ‘Mbunge Nje ya Bunge’ nitaendelea kushirikiana nao kwa sababu bado nina wito na ninaipenda Mikumi, mwaka 2025 nitarudi tena kugombea pale sababu nina ajenda zangu niliifikisha Mikumi sehemu na sijamalizia.

 

 

“Mwana 2025 huenda nisigombee ubunge tu, huenda nikagombea hata Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa sababu nina ndoto kubwa.

 

“Mstari wa ‘mchozi mengi machoni, fedha chache mfukoni’ Nimefurahi Serikali kuondoa tozo kwenye YouTube channel za wasanii sababu ilikuwa unakuta msanii ndio anaanza hana hata mia halafu unamwambia alipie Tsh mil 1, lazima azirai. Kwa sasa mambo yanakwenda kuwa safi.

 

 

“Nachoweza kuishauri Serikali ni kuboresha Sheria za kulinda kazi za wasanii, kutafuta masoko na mfumo mzuri wa kusajili wasanii wajulikane wako wapi wanafanya nini, hii itaiongezea pia Serikali kupata mapato. Serikali ipate na msanii apate, la sivyo tunapoteza time,” Prof. Jay.

Leave A Reply