The House of Favourite Newspapers

Yanga Wamuandalia Saido Mwaka Mmoja

0

YANGA wajanja sana, fasta wamefikia makubaliano mazuri na kiungo wao mshambuliaji Mrundi Said Ntibazonkiza ‘Saido’ kwa ajili ya kumuongezea mkataba mwingine wa kuendelea kukipiga Jangwani.

 

Saido ni kati ya wachezaji wa Yanga ambao mikataba yao inatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu pamoja na wenzake Said Makapu, Deus Kaseke, Adeyum Saleh na Fiston Abdoulrazack.

 

Staa huyo mpya ndani ya Yanga alijiunga na timu hiyo katika usajili wa dirisha dogo kama mchezaji huru akisaini mkataba wa miezi sita.

 

Championi Jumatano, limejiridhisha kuwa Yanga imekubaliana na kiungo huyo kumuongezea mkataba wa miaka miwili, licha ya yeye mwenyewe kuomba apewe mwaka mmoja pekee.

Kwa mujibu wa mmoja wa mabosi wakubwa wenye ushawishi mkubwa ndani ya Yanga, huenda wakafikia muafaka mzuri wa kumuongezea mkataba huo ndani ya wiki mbili na kusaini baada ya yeye mwenyewe kuonyesha nia ya kubakia Jangwani.“Saido ameonyesha ukomavu na umuhimu wake ndani ya timu kwa muda mfupi tofauti na washambuliaji wengine wa kimataifa.

 

Hivyo tumeona ni vema tukamuwahi mapema kumuongezea mkataba kabla ya kuchukua maamuzi ya kuondoka.“Ukiangalia kiwango na uwezo ambao wameonyesha washambuliaji wetu Sarpong (Michael) na Fiston (Abdoulrazack) ni mdogo sana, hiyo inatufanya sisi viongozi tusitishe mikataba yao.

 

Lakini kwa Saido yeye tunashawishika kumuongezea mkataba mpya kwani katika michezo mitano ameasisti mara nne na kufunga mabao mawili, kiukweli takwimu zinaongea kwake hivyo hatuoni sababu za kutomuongezea mkataba mpya,”alisema bosi huyo.

 

Alipotafutwa Mwenyekiti Mkuu wa Klabu ya Yanga Dk Mshindo Msolla kuzungumzia hilo alisema kuwa “Ni mapema kuzungumzia suala la usajili, kwani hivi sasa viongozi akili zetu tumezielekeza katika michezo iliyobakia lakini ni ngumu kumuachia Saido katika timu yenye malengo.

WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

Leave A Reply