The House of Favourite Newspapers

JPM: Matusi Nayotukanwa Nayafurahia, Wanamchukia Kigwangalla kwa Sura – Video

0

Mgombea Urais kwa Tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli amefanya mkutano na wananchi wa Nzega mkoani Tabora kwenye kampeni zake za Urais leo Jumatano, Septemba 2, 2020.

 

Akizungumza wakati wa kampenzi hizo zilizofanyika katika Uwanja wa Parking, Nzega Mjini, Magufuli amesema Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka huu yenye kurasa 303, imesheheni mambo mengi ya kuyafanya huku akieleza kuwa wapo watakaokuja kuyaharibu kwa kuwa hawajui hata fedha anazitatoka wapi, na wapo wanaoamini hela lazima zitoke Ulaya, wakati hela ipo hapa na imekaliwa na mafisadi.

 

“Mimi nilienda Ulaya nikiwa nasoma na tangu nimechaguliwa kuwa Rais sijawahi kwenda Ulaya kwa sababu Ulaya ipo hapa. Nataka niitengeneze Tanzania kuwa Ulaya. Hakuna sababu ya kwenda kupanda ndege za Ulaya wakati uwezo wa kununua ndege unao. Mturudishe tena mtupe miaka mitano mingine muone maajabu tutakayoyafanya kwa wananchi wa Nzega na mkoa mzima wa Tabora.

 

“Tanzania tuna mambo mengi ya kufanya na ndiyo maana nachagua vijana ili wanisaidie. Nafahamu changamoto za nchi hii ni nyingi. Kwenye elimu watoto walikuwa lazima walipe ada hata kama ni masikini. Leo watoto wanaoingia Msingi na Sekondari wameongezeka.

 

“Mimi nawaomba kura Watanzania wote. WanaCCM, wanaCHADEMA, wanaCUF ninawaomba kura. WanaACT nawaomba kura hata wale ambao hawana chama, kwa sababu ninaamini maendeleo hayana chama, haya maji yanayokuja watayatumia watu wa vyama vyote.

 

“Niwaletee maji, nihangaike usiku na mchana leo mseme hapana, nitaumia lakini nitamshukuru Mungu. Hata nilipokuwa Waziri wa Ujenzi hata nilipopitisha barabara mkasema mbona anapitisha kule mbali, lakini ukiwa kiongozi ni lazima ukubali lawama.

 

“Tumeamua umeme usiwe kwa matajiri tu bali umeme uende kwa kila mmoja ilimradi ni Mtanzania. Katika kipindi cha miaka 5 tumepeleka umeme kwenye Vijiji 9,570. Ifikie kila Kijiji kiwe na umeme na hata katika kuweka umeme hatuchagui.

 

“Matusi ninayotukanwa mimi nayafurahia kwasababu naona ni sadaka ya kuwatumikia Watanzania. Wale tuliowanyima nafasi za kuiibia Tanzania hawawezi kufurahia. Matusi niyapate lakini ninyi mpate maendeleo ya kweli kwa faida ya Watanzania wote kwa ujumla.

 

“Inawezekana watu wakamchukia Kigwangalla kwa sababu ya sura yake, lakini hata mimi sura yangu mbaya tu. Ukitaka sura nzuri basi katafute mke wako au mume wako. Hapa sisi tunataka kazi.

 

“Wapo wengine tukiwapa nafasi watachukua vitu vyetu wapeleke Ulaya maana wamezoea kukaa Ulaya. Mimi nimeenda Ulaya wakati nasoma lakini tangu niwe Rais sijaenda Ulaya nataka niitengeneze Tanzania iwe kama Ulaya ili wa Ulaya waje Tanzania.

 

“Hakuna anayeweza kufanya niliyofanya na viongozi wenzangu, hao wengine watakuja kuharibu tu, hawajui hata hela zinatoka wapi. Wapo wanaoamini hela zinatoka Ulaya, wakati zimekaliwa hapa na Mafisadi na anayeweza kupambana nao ni mimi na wenzangu.

 

“Maji ni muhimu, maji ni uhai. Ukitaka kula maji muhimu, ukitaka kufua maji muhimu, ukitaka mke wako akupende maji ni muhimu, ukitaka mumeo akupende maji muhimu. Leo maji tumeyafikisha Tabora kwa 95%. Nitashangaa Wananchi wa Nzega mkininyima kura.

 

“Tanzania tuna mambo mengi ya kufanya na ndiyo maana nachagua vijana ili wanisaidie. Nafahamu changamoto za nchi hii ni nyingi. Kwenye elimu watoto walikuwa lazima walipe ada hata kama ni masikini. Leo watoto wanaoingia Msingi na Sekondari wameongezeka.

 

“Katika mchakato wapo ambao hawakushinda wengine wamenuna. Nawaomba wasinune, kama kununa kamnunie mkeo au mumeo nyumbani. Mkawaunge mkono waliopitishwa, tukisusa tunakiumiza Chama. Vyeo vipo vingi unaweza kukosa Udiwani ukapata Ukuu wa Wilaya,” amesema Magufuli.

 

Leave A Reply