The House of Favourite Newspapers

Magufuli: Mishahara Madini Ipunguzwe – Video

0

RAIS  John Magufuli, leo Desemba 12, amemwapisha, Profesa Shukrani Manya, kuwa Naibu waziri wa madini. Naibu waziri wa madini huyo, ameteuliwa baada ya yule wa awali, Francis Ndulane, kushindwa kuapa.

 

“Siku tulipokuwa tukiwaapisha mawaziri na manaibu, makamu wa rais aliwadokeza kwamba reserve tunao wengi, kwa hiyo wachezaji mliochaguliwa mkachape kazi, tumekuchagua wewe kwa sababu wizara hii tuliona kwenye nafasi za juu inayumba.

 

“Sekta ya madini ni muhimu sana mkijipanga vizuri, mkiamua sekta ya madini inaweza ikatoa mchango mkubwa sana katika taifa, ni lazima mjiulize Tanzania tuna madini ya kila aina, tuna chuma, kwa nini hii chuma isiyeyushwe ikatengenezwa nondo?

 

“Tume ya Madini kafanyeni kazi, ninafahamu kuna matatizo madogo wale watu wetu tuliowapunguza wapo hapa, nataka nilizungumze hapa ili msije mkatafuta mchawi, wa TMAA (Wakala wa Uchunguzi wa Madini) mlikokuwa kule mlikuwa na mishahara mizuri kile kitengo tulikifuta.

 

“Ile mishahara Katibu Mkuu Kiongozi ipunguzwe sababu kazi waliyoifanya TMAA ilikuwa ya hovyo, ulitoka kule na mshahara wa mil. 10 ukamzidi hata mkurugenzi wako, anayetakiwa kuzidiwa ni mimi napata mshahara Mil. 9 lakini mtu wa TRA ana Mil. 15,” alisema Magufuli na kuongeza:

 

“Nilikuwa nasikia kwenye vyombo vya habari vya kimataifa kwamba kuna sehemu watu 3,000 wamekufa siku moja kwa Corona, sisi Tanzania tuna wajibu wa kumshukuru Mungu kwa upendo mkubwa, Watanzania tuendelee kumshukuru kwa kutuokoa na Corona.

 

“Mimi najua Mungu ataendelea kutusimamia kwa sababu tunaambiwa shukuruni kwa kila jambo, Mungu amefanya miujiza katika taifa letu ili kusudi mataifa ambayo hayataki kumuamini Mungu yamuamini siku moja kwamba anaweza akafanya maajabu.”

 

Leave A Reply